Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi Prof. Herson nonga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kongamano la Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.
Mganga Mku wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akiongea na waandishi wa habari (hawapo kwenye Picha) mara baada ya kufungua kongamano la wiki ya usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.
Wadau na washiriki wa kongamano la wiki ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa wakifuatilia mijadala mbali mbali iliyokuwa ikijadiliwa katika kongamano hilo mara baada ya ufunguzi.
………………………………….
Hayo yamesemwa leo Dar es salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Tumaini Nagu kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati wa ufunguzi wa kongamano la afya shirikishi kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa lililowakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya afya.
Amesema kwamba Serikali inatekeleza mkakati wa 68 wa kidunia wa mkutano wa afya uliofanyika mei 2015 ambapo Mkutano huo uliweka Mazimio kwa nchi wanachama wa ndani kutekeleza mpango kazi kwa kutumia mfumo shirikishi wa kukabiliana na janga la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
Profesa. Nagu amesema kuwa mpango kazi huo una ainisha malengo makuu matano ya kimkakati yakupunguza usugu huo ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa vimelea sugu pamoja na matumizi sahihi ya dawa za antimicrobial ili kuhakikisha hatua za kukabiliana na janga hilo.
Amesema kuwa katika kutekeleza mpango kazi wa kitaifa wa 2017 /2022 Wizara ya Afya imefanikiwa kutekeleza kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo,Mifugo,nakwamba serikali kupitia Wizara ya Afya imeweza kufanya maboresho mbalimbali kupitia maabala zake kwa kuweza kufanya tafiti juu ya vimelea sugu dhidi ya dawa.
Amesema kwamba Sekta ya Afya imeweza kuandaa sampuli mbalimbali nakuzipeleka maabara vya ajili ya kufanya utafiti.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wanyama Nchini ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa .Hezron Nonga amewashauri Watanzania kuhakikisha wanawapatia matibabu Wanyama wao kwa kutumia wataalamu wa mifugo( maafisa mifugo) ili kupunguza tatizo la uwezekano wa kuambukiza binadamu wanaotumia kitoeo cha nyama.
Nae Mwakilishi kutoka shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Rose muhangwa shija amesema kuwa mwaka 2019 vifo milioni 4.95 duniani kote vilitokana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa nakwamba Vifo zaidi milioni 1 hutokea ndani ya mwaka mmoja hivyo kuna haja kila nchi kutoa elimu ya kutosha wa wananchi wake kuhusu Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa ili kupunguza madhara makubwa zaidi yanayoweza jitokeza.