Meneja wa Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi Victoria Msina (kulia) akizungumza na mwananchi aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo kupata Elimu na kujionea shughuli zinazofanywa na Benki hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyoanza rasmi leo Novemba 21.2022 katika viwanja vya Rockcity Mall Jijini Mwanaza.
Bi Victoria Msina Meneja wa Mawasiliano wa BoT (wa kwanza kushoto) akiwa na Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha Deogratias Mnyamani (wa pili kushoto) wakiwasikiliza wananchi waliofika kwenye Banda la Benki hiyo kupata Elimu.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha Deogratias Mnyamani akitoa mafunzo kwa wajasiriamali na wadau mbalimbali zaidi ya 200 kuhusu umuhimu wa kuweka akiba. Semina hiyo imefanyika leo Novemba 21,2022 katika viwanja vya ‘Rock city Mall’ Jijini Mwanaza.
Wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya fedha katika Maonesho hayo.
Mhasibu Mwandamizi wa BoT tawi la Mwanza Bi. Claudia Manyanda (kushoto mwenye fulana nyekundu) akizungumza na wananchi waliotembelea kwenye maonesho hayo leo Novemba 21, 2022 Jijini Mwanza.
Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Miriam Mgina akitoa elimu ya utambuzi wa pesa bandia kwa mwananchi aliyefika kwenye Banda la Benki hiyo kupata elimu.
Maafisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Grayson Nyenga (wa kwanza kulia), Gideon Rwegoshora (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Benki hiyo Bi. Rukia Muhaji (wa tatu kulia) wakimsikiliza moja ya mwananchi aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo kupata elimu na kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki hiyo.
MWANZA.
Wito umetolewa kwa watanzania kuwa na utaratibu wa kuweka akiba itakayowaezesha kufikia malengo yao ya kiuchumi.
Wito huo umetolewa leo Novemba 21,2022 na Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Deogratias Mnyamani alipokuwa akitoa mafunzo kwa wajasiriamali na wadau mbalimbali zaidi ya 200 kuhusu umuhimu wa kuweka akiba katika semina iliyoandakiwa na Wizara ya fedha na mipango katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Jijini Mwanza.
Mnyamani ameeleza kuwa BoT ina jukumu la kuuelemisha umma kuhusu umuhimu wa kuweka akiba na kwamba watu wengi wamekosa elimu hiyo ya Uwekezaji wa Akiba.
“Akiba ni utamadun ambao mtu anaujenga na inakuwa sehemu ya maisha yake kwamba kila pesa anayoipata kabla hata ya kufikiria changamoto zinazomkabili aanze kwanza kufikiria kuweka akiba”amesema Mnyamani.
Amesema kuwa kama wananchi wote ususani vijana wataweza kuwa na utaratibu wa kuweka akiba kwenye maeneo salama yanayotambulika na serikali na wakaanza kuuzoea taratibu huo watakuwa na uchumi mzuri kiakiba hapo baadae.
“Tunawaelekeza na kuwafundiaha kuweka akiba sehemu zinazotambulika na Serikali hususani zinazosimamiwa na Benki Kuu ambayo ni Benki za Biashara, Benki ndogo za jamii, kwenye saccos, vyama vya ushirika vya akiba na mikopo na kwenye vikundi vya huduma ndogo za fedha” amesema.
Pia ameongeza kwa kuongelea umuhimu wa kuweka pesa kwenye maeneo ambayo pesa zao zitakuwa zikiongezeka kwa wakati maalum na kwamba zipo taasisi zinatoka riba kulingana na muda ambao umewekwa kulingana na vegezo na masharti tofauti na taasisi husika ambapo amewashauri wajasiriamali hao kuangalia vigezo na masharti kama zinaendana na matakwa yao kabla ya kufanya maamuzi ili kufikia malengo yao.
“Changamoto kubwa ambayo tunaiona kwa sasa ni elimu ya namna ya kujiwekea akiba na ndio maana Serikali kupitia Wizara ya fedha imeamua kufanya Maonesho haya ili kutoa elimu kwa wananchi kwani ikiwa atapata taarifa sahihi ataweza kufanya maamuzi sahihi na itamsaidia kujua mahali sahihi pa kwenda kuweka akiba yake” ameongeza.
Hata hivyo Mnyamani amesema kuwa kwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kuwa na watoa huduma wengi katika sekta ya fedha iliyosambaa nchi nzima ambayo imetoa urahisi mkubwa kwa wananchi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati.