Na Dotto Mwaibale, Singida
MKURUGENZI wa Maadhimisho na Sherehe
za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomeo Jungu
amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimaliwa Watu na
Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu kushindwa kufuata Itifaki
na Uratibu wa matukio ya viongozi wa kitaifa.
Jungu ameyasema hayo jana mkoani
Singida kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa
Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na
Rasilimali watu.
Alisema kuna baadhi ya Wakurugenzi
wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na
Rasilimali watu hawajui hata mavazi ya kuvaa pale kunapokuwa na viongozi wa
kitaifa, huku wengine hawajui hata namna ya kula mbele ya viongozi wa kitaifa.
Aidha alisema mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki kwenye
matukio ya viongozi wa kitaifa kwa wakurugenzi yanatajwa kuwasaidia wakurugenzi
hao kujua itifaki viongozi wa kitaifa wanapofika katika maeneo yao ya utendaji.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Ezavier Daud alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuondoa au
kupunguza changamoto zinazojitokeza katika masuala ya itifaki kwa Wakurugenzi
wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa sehemu ya Utawala na
Rasilimali watu.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alitoa wito kwa wakurugenzi hao na makatibu
tawala wasaidizi kuyatumia mafunazo haya kuwa suluhisho la makosa
yanayojitokeza kwenye suala la itifaki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo haya wamesema mafunzo hayo yatawasaidia
kujua kujua itifaki Kwenye matukio ya viongozi wa kitaifa wanapotembelea maeneo
yao.