……………..,….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
ZAINABU Vullu ameshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani baada ya kupata kura 320 dhidi ya kura 38 za mshindi wa pili Joan Tandau.
Akitoa matokeo katika uchaguzi wa Umoja wa wanawake wa CCM Mkoani Pwani, msimamizi wa uchaguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdala, alisema upande wa mwakilishi wa baraza kuu la mkoa kwenda Taifa Mariamu Ibrahimu ameshinda kwa kupata kura 188 akimshinda Nancy Mutalemwa aliyepata kura 165.
Alimtaja Dk .Zainabu Gama kuwa kaibuka kidedea kwa kushinda nafasi ya Mjumbe kutoka UWT kwenda Jumuiya Mkoa, na mwakilishi kwenda mkutano mkuu CCM Mkoa ni Meri Nchimbi, Mariamu Ibrahimu kutoka UWT kwenda Baraza Kuu Taifa.
Akitoa shukran kwa wajumbe ,Mwenyekiti wa UWT Pwani Zainab Vullu alisema ,umoja na mshikamano ni nguzo kubwa katika Jumuiya hiyo,hivyo amewataka wanawake kuungana ili kuimarisha Jumuiya.
Aidha aliahidi kufuatilia suala la asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya ili ziweze kusaidia makundi yanayolengwa wakiwemo wanawake wapate fedha hizo kwa wakati.