Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amehudhuria katika Mkutano wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mabalozi wa Tanzania unaoendelea katika Hotel Verde, Zanzibar. Katika Mkutano huo Mshomba akiwa ni mjadili mada alipata muda wa kuzungumzia masuala ya uwekezaji na fursa zilizopo NSSF. Mjadala huo ulitanguliwa na wasilisho kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba. Awali wageni mbalimbali walitembelea Banda la NSSF akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax, Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia Mhe. Dkt. Ramadhan Dau na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi James Bwana.
NSSF inatumia Mkutano huo kwa ajili ya kutangaza Fursa mbalimbali za Uwekezaji ikiwa ni mradi wa nyumba za kisasa, miradi ya uwekezaji ya jengo la Mzizima Tower, jengo la hoteli Mwanza pamoja na viwanja.