Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula nakala ya Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) baada ya kuzindua Sera hiyo kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi nakala ya Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumbna la Taifa (NHC) baada ya kuzindua Sera hiyo kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC nakala ya Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumbna la Taifa (NHC) baada ya kuzindua Sera hiyo kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. Katiakati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakionyesha nakala za sera hiyo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dkt. Sophia Kongeli na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akizungumza wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.
Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC akizungumza wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.
Picha zikionesha wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa sera hiyo uliofanyika kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius. Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.
Shirika la Nyumba la Taifa NHC limezindua rasmi sera ya ubia katika ya shirika hilo wakishirikiana na sekta binafsi ambapo sera hiyo imefanyiwa maboresho mbali mbali, shirika hilo limeeleza kutoingia ubia na sekta binafsi zaidi ya miaka (10)likuwa ni pamoja na kuangalia Sera ambayo inaweza kuvutia wawekezaji na kukuza pato la Taifa.
Mkurugenzi wa shirika hilo ndugu Nehemia Mchechu amesema hayo leo alipokuwa anzungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo amesema kwamba shirika hilo limefungua milango kwa wawekezaji mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
“Leo tumeanzia hapa Dar es salam tuna wiki tatu za kuelimisha na kufanya mafunzo kila wikiendi kwa wafanya Biashara kuwaeleza nini kinafanyika katika sera hii baada ya hapo tutakuwa na zoezi hili kwenye baadhi ya mikoa mikubwa kama Mwanza na Arusha lakini baadae tutangalia ratiba ili tuweze kuwafuata baadhi ya Wawekezaji wa nje ya Nchi,”
Amesema Mchechu.
Aidha Mchechu ameongeza kwamba sekta hiyo ina manufaa mengi sana kwani kila mmoja wetu anahitaji nyumba bora kwa ajili ya kuishi na kwa sasa Watanzania Wapo wengi hivyo shirika pekee haliwezi kujenga nyumba za kutosheleza uhitaji ndio maana ndiyo maana kama NHC limeamua kushirikisha sekta binafsi katika miradi yake.
Ameongeza kwamba shirika hilo linaendelea na mradi wa “Samia House Scheme” ambapo nyumbani hizo zinajegwa Kawe na mwezi ujao zitaanza kujengwa Dodoma na mikoa mingine lakini pia miradi yote itaendelea bila kusita, shirika hilo pia limehaidi kufanya vikao na benki mbali mbali ili wawe tayari kuwakopesha Wajenzi pamoja na wanunuzi wa nyumbani hizo wenye vigezo vinavyotakiwa.
Kuhusu sera za uwekezaji shirika la nyumba limeweka sera rafiki ambazo zipo wazi na mwekezaji atakaa na kukubaliana na shirika kabla ya kuanza kuwekeza.
Shirika hilo limewatoa hofu wawekezaji kwa kusema kwamba wawekezaji wote watakaofika ofisini kwao kwa nia ya kufanya uwekezaji kwenye miradi wataelimishwa namna bora ya kuwekeza bila utapeli wala kuzungushwa kwa namna yeyote ile ili miradi iweze kufanyika kwa wingi kuongeza pato la Taifa kwa maslahi ya Watanzania.