…………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana leo tarehe 10 Novemba 2022 ameshiriki kikao cha dharura cha Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichojadili na Kuidhinisha Mwongozo wa Kuandaa Msimamo wa Nchi za SADC katika utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa ya masuala Uhifadhi ya Mazingira.
Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao pia kimejadili na kuidhinisha mpango mkakati wa ushirikiano wa SADC 2022-2025, na Waraka kuhusu msimamo wa pamoja wa nchi za SADC katika Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa CITES utakaofanyika nchini Panama.
Aidha, kikao hicho kimeidhinisha Waraka wa msimamo wa pamoja wa nchi za SADC katika Mkutano wa 19 wa CITES.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka sekta ya Wanyamapori.