……………….
MKURUGENZI wa Taasisi ya urembo nchini Maznat Bridal Bi Maaza Senare amewataka wadau wa sekta ya ubunifu na sanaa kushiriki katika kuwasaidia vijana na mabinti katika mitaa kutumia fursa na vipaji vyao kujipatia ajira rasmi badala ya kuwaacha katika vijiwe ambako hukutana na hatari za athari ya madawa ya kulevya kutokana na kukosa Kazi za kufanya
Maaza ameyasema hayo kwenye mahafali ya tatu ya chuo hicho kilichopo jijini Dar Es Salaam na mwaka huu 2022, wanafunzi 178 wamehitimu katika fani mbalimbali kutoka katika mikoa ya Iringa, Chato, Morogoro, Singida na Dar Es Salaam na tayari baadhi ya wahitimu wameshapata ajira kupitia kazi za urembo na utanashati
“Natoa wito kwa serikali na jamii kwa ujumla kuheshimu Kazi za urembo na msiwaache watoto wenu wamekaa bure wakati Kazi zipo nyingi katika kila kaya, watu wanasuka, kutengeneza kucha, kunyoa pamoja na huduma zingine ambazo zinahitaji kada hii muhimu” alisema
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Anold Kinyaiya amesema serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kuwasaidia wadau wa ubunifu nchini, japo zipo changamoto chache ambazo zinaikabili sekta ubunifu ikiwa na pamoja na uhaba wa mitaji, lakini serikali itashirikiana na wadau wakati wowote kwenye masuala ya Maendeleo