Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akifungua mafunzo ya viongozi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni mwenzeshaji wa mafunzo hayo Prof Silvia Temu na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi Nuru Sovellah.Mkurugenzi wa Makumbusho ya Azimo la Arusha, Dkt Gwakisa Kamatula akitoa shukrani kwa mafunzo hayoMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga akimkabidhi zawadi Prof. Silvia Temu baada ya kukamilisha mafunzo hayoBaadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini
…………………
Na Mwandishi Wetu
Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa imefanyiwa mafunzo ya uongozi ili kuimarisha utendaji kazi na uhifadhi wa urithi wa asili na utamaduni.
Mafunzo hayo yalijumuisha viongozi wote wa vituo, idara na vitengo vya Makumbusho na Malikale nchini yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo yamendeshwa na Prof. Silvia Temu ambaye ni mtaalamu mbobezi katika masuala ya uongozi nchini.
Mafunzo hayo yalijuisha masuala mbalimbali ya uongozi ikiwemo sifa za kiongozi bora, mchango wa menejimenti ya Taasisi katika utendaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi, kufanyakazi kwa ushirikiano (teamwork) na utunzaji wa muda katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mtaalamu wa Mafunzo hayo Prof. Silvia Temu ameitaka menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kufanyakazi kwa weledi na kwa kushirikiana huku wakiukomboa wakati.
“Wakati ni mali jipangie majukumu yako na tekeleza kwa weledi kwa kukomboa wakati alisema Prof Temu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga alimshukuru Prof. Temu kwa mafunzo hayo ambayo yalilenga katika kuiweka tayari menejimenti yake katika kutekeleza maagizo mbalimbali yatakayotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa iliyozinduliwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Kituo cha Azimio la Arusha, Dkt Gwakisa Kamatula akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga viongozi hao wa jinsi ya kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.
“ Tunashukuru kwa mafunzo haya mazuri yatakayotusaidia katika kuboresha utendaji wetu wa kazi katika vituo, idara na vitengo vyetu,” alisema Dkt Kamatula.
MWISHO