Na
Mwandishi Wetu, Arusha
AFISA Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka Vijana mkoani
Singida na Wananchi kwa ujumla kuwekeza katika Kilimo cha Viazi Lishe.
Ndahani
ameyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akifunga mafunzo ya Kilimo cha viazi,maharage,mahindi lishe na kuyaoyaongezea thamani mazao hayo kwa Vijana 12 kutoka mkoani Singida walioenda kujifunza kwa udhamini wa Shirika la Chakula Duniani
(FAO-Tanzania) Chini ya Mradi wa kuwawezesha Vijana kujiajiri katika
Kilimo Biashara.
Ndahani
alisema Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa inayozalisha viazi vitamu kwa
wingi,lakini elimu ndogo ya wakulima juu ya uhifadhi wa mbegu za viazi,uchaguzi
wa mbegu ,kilimo cha kisasa,uvunaji na uongezeji wa thamani zao hilo imekuwa
tatizo,mfano mwaka jana wakulima wengi hawakupata mavuno kwa sababu ya kuchelewa
kupanda viazi wakisubiri mvua za kwanza ambazo hutumika kama mvua
za kukuzia mbegu ya viazi.
Kutokana
na mafunzo hayo Vijana wa Singida watalima kisisa kutokana na mbegu ya viazi lishe ambavyo vina soko kubwa kutokana na kuwa na
virutubisho vingi vinavyowasaidia watoto,wazee na wajawazito.
Ndahani
alisema endapo Vijana wa Singida wakajikita katika Kilimo cha Viazi Lishe
tatizo la ukosefu wa ajira na utapiamlo litakoma katika mkoa huo ambapo amewaomba vijana kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao binafsi,moa na Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MBC, Zena Mshana alisema vijana hao wamejifunza kwa muda wa mwezi
mmoja Kilimo cha Viazi Lishe, Maharage Lishe na Mahindi Lishe pamoja na
uongezeji wa thamani wa mazao hayo na kueleza watakuwa na uwezo wa kuanzisha miradi
ya kilimo na kuwa wakulima wakubwa..
Aidha
alisema wameamua kujikita katika kilimo cha mazao lishe ili kuondoa tatizo la
utapiamlo ambao unawakuta watoto hasa wenye miaka 0 hadi 5.
kiongozi wa vijana hao Mvanga Juma Mohammed akizungumza kwa niaba yao ameishukuru Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa, Shirika la Fao na MBC Enterprise Ltd kwa kuwapatia mafunzo
hayo ambayo yamekuwa wa tija kwa vijana na kuahidi kuwa watatoa elimu kwa vijana wenzao na wakulima wa viazi na maharage lishe mkoani Singida ili kufanya kilimo chenye tija katika maisha yao na Taifa kwa ujumla kwani wanaamini kilimo
pekee ndicho kinaweza kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.
Mohamed amemuomba Waziri wa Kilimo kuweka mkakati mzuri wa kuwawezesha vijana kupata
mbegu ,mbolea na maeneo ya kilimo kwa vijana nchini pia TARI kuhakikisha mbegu
ya Maharage Lishe Aina ya TARI 14
na 15 zinapatikana kwa urahisi.