………………….,..
KAMISHNA msaidizi wa Ardhi kanda ya Dar Es Salaam Idrisa Kayera ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuzitumia vizuri kliniki zilizoanzishwa na Wizara ya Ardhi ambazo zitasaidia kutatua migogoro katika ngazi za chini na kuleta Maendeleo badala ya kusababisha malumbano katika mabaraza ya Ardhi na kusababisha hasara kubwa kitu ambacho kinazorotesha ukuaji wa uchumi katika ngazi mbalimbali
Kayera ameyasema hayo Jijini Dar Es Salaam wakati wa zoezi la ugawaji Hati kwa wananchi zaidi ya 200 katika Manispaa ya Ubungo
Amesema uwepo wa kliniki hizi utasaidia wananchi wengi kuacha mivutano isiyo ya lazima kwenda kwenye mabaraza ya Ardhi na kuendelea na uzalishaji mwingine wenye tija zaidi
“natoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam kujitokeza kuchukua Hati lakini pia kutatua migogoro iliyo katika ngazi za chini, ifike mahala wananchi waelewe taratibu za umiliki wa Ardhi na kwa bahati mbaya migogoro mingi inatokana na uelewa Mdogo hususani ngazi za mitaa” alisema
Kwa upande wake mkuu wa idara ya Mipango miji Fadhiri Hussein amesema maeneo mengi yameshapimwa na wananchi wanachelewa kuchukua Hati kutokana na viambatanisho muhimu kukosekana, ametoa mfano wa namba za NIDA ambazo zinasaidia uwepo wa taarifa muhimu katika milki ya mtu, “kila mwananchi mwenye Hati anapaswa kuja na kitambulisho au namba za NIDA ili kurahisisha zoezi letu la kurasimisha vipande vya Ardhi katika manispaa ya Ubungo
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Saranga Godwin Muro amekemea baadhi ya wenyeviti kujiingiza katika mauziano ya viwanja na kuchafua taswira nzuri za wenyeviti kwa kudai pesa za asilimia kumi huku wakijua ni kinyume na taratibu za mauziano, serikali kupitia Wizara ya Ardhi ilishaelekeza majukumu ya wenyeviti katika mauziano yatasalia kwenye kuwatambulisha wakazi wetu kwa wenye mamlaka ya kusimamia manunuzi lakini si kuwa sehemu ya manunuzi au kulazimisha wananchi kutoa fedha, alisema