Tamasha kubwa la kuliombea taifa linatarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe 6 mwezi Novemba 2022 katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani mwanza ambaoo waimbaji wa injili kutoka mataifa mbali mbali watatumbuiza.
Waandaaji wa tamasha hilo Msama Promotion wamesema kuwa taratibu zote zimeshakuwa tayari na wachungaji, maaskofu mbali mbali watahudhuria katika tamasha kwa lengo la kuiombea Taifa na kumuombea mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan huku mgeni ramsi akitarajiwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Aidha mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo Bw. Emmanuel Mabisa ameeleza kuwa tamasha hilo litaanza Asubuhi saa mbili ambapo kiingilio ni shilingi elfu mbili (2000) kwa wakubwa na watoto ni shilingi elfu moja (1000)
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose mhando amesema siku ya jumapili ya tarehe sita(6) ni siku maalum kabisa ambayo wameitenga kuliombea Taifa na kumuombea Rais Sami Suluhu Hassan na kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuliongoza vyema taifa letu ya Tanzania.
Tumepita katika wakati mgumu sana lakini Rais wetu ametubeba kama familia yake mgongoni na kuhakikisha tunavuka wote salama kama mstari wa bibilia unavyosema kwamba mama aliehodari hutoka asubuhi na mapema akienda Jagwani kutafuta chakula, Rais wetu amepambana ameigiza Royal Tour ambayo imesababisha kuongezeka kwa watalii na kuongeza kipato cha nchi, kuongeza ajira kwa Vijana lakini pia kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kimataifa ndio maana sisi tumeamua kufanya tamasha hili la kumwombea na kumshukuru,
Amesema
Mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili Rose mhando ametumia nafasi hiyo pia kumshukuru Rais kwani Samia Suluhu Hassan kwani kwenye utawala wake wameweza kupata mirahaba ya kazi zao kitu ambacho hawakuwahi kupata kipindi cha nyuma.
Aidha wananchi kutoka mkoa wa mwanza na mikoa ya jirani wanakaribishwa kushiriki katika tamasha hilo la historia.