OR – TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Sillinde amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi million 475 kwaajili ya ujenzi wa barabara itakayounganisha vijiji vya Muungano, Mikocheni na Chemchem
Akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua serikali inampango gani wa kujenga daraja kata ya Arusha chini litakalo unganisha vijiji vya Muungano, Mikocheni na Chemchem Mhe. Silinde amesema mradi huo upo kwenye hatua za manunuzi kwa ajili ya kupata mkandarasi
Aidha, amesema Serikali imeweka mkakati wa kutambua madaraja yote korofi katika maeneo yote ambayo yanaitajika kuhudumiwa ili kuunganisha eneo moja na lingine.
Pia Mhe. Sillinde ameeleza kupitia TARURA serikali itaendelea kuweka vipaumbele kulingana na utafutaji wa fedha ili kuakikisha barabara zote zinaweza kupitika katika kipindi chote cha mwaka.