Waziri Mkuu kasimu Majaliwa amezindua mradi wa kisima na tanki la kuhifadhi maji wilaya ya kigamboni alipokuwa kwenye ziara ya kutekeleza agizo la Rais Samia suluhu Hassan la ukaguzi wa miradi ya maji.
Amesema Jiji la Dar es salam kwa sasa limekuwa na upungufu mkubwa wa maji huku akisema mkoa wa Dar es salaam unahitaji lita za maji milion mia tano na arobaini(540) kwa siku ambapo kwa sasa kutokana na ukame uliopo na hali ya mto Ruvu maji kupungua hivi Mkoa wa Dar es salam unapata lita milion mia tatu pekee.
Aidha amesema kuwa Dar es salaam ina upungufu wa lita mia mbili na ishirini ambapo kupitia mradi huo aliozindua leo Kigamboni kata ya Kasarawe ll utapunguza uhaba wa maji katika Wilaya ya kigamboni na Wilaya jirani ya temeke na kinondoni.
“Leo nimekuja kuzindua kisima ambacho kilikuwa kwenye uchimbaji na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji nakwamba tayari maji hayo yameanza kuingia kwenye tanki ambalo tunatarajia litaingiza maji lita milion sabini hivyo maji hayo yatatumika kigamboni na Wilaya za jirani”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa bonde la maji ya Mto Ruvu kushirikiana na Wananchi kuhakikisha maeneo yote yenye vyanzo vya maji kulindwa, ikiwa ni pamoja na kuacha kukata miti hovyo ‘ pia kuacha kuchunga mifugo katika vyanzo vya maji.
Ameongeza kwamba endapo Mamlaka husika hazitafanya kazi ya kuulinda mto Ruvu kuna uwezekano wa Mkoa wa Dar es salam usipate maji yakutoshereza huku akitolea mfano Mkoa wa Morogoro , Tanga (Handeni) na Mkoa wa Mbeya inaweza kuathirika kutokana na mikoa hiyo kujitegemea maji ya mto Ruvu.
Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa Dawasa ndio mwenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba maji zaidi ya lita milioni mia tano na arobaini yanapatikana kwani wananchi wanahitaji kuwa na ziada ya maji kukabiliana na dharura inapotokea.
“Katika jitihada alizozifanya Mwaka jana Rais Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi Bilion ishirini na tano kwa ajili ya kuchimba visima kumi(10) ni jitihada ambazo pia mamlaka husika kupitia mapato yake kutenga fedha na iendelee kuchimba visima zaidi”amesema Majaliwa
Wziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa Dawasa kumalizia mradi wa visima vitatu ambavyo uchimbaji wake bado haujakamilika akiwataka wawachukue wataalam kutoka chuo cha Maji kwenda kumalizia uchimbaji huo, ambapo Waziri Majaliwa pia ametoa pendekezo kushirikishwa kwa sekta binafsi katika uchimbaji wa visima kwa lengo la kupatikana wa maji ya kutosha.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Amos Makalla amemshukuru Waziri Mkuu kwa uzinduzi wa kisima na tanki ambapo visima saba kati ya kumi vimekamilika kutokan na fedha shilingi bilioni 25 ambazo zilitolewa na Rais Samia.
Makalla ameahidi kushirikiana na viongozi wa Wilaya kulinda Mradi huo kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salam nakwamba Miradi yote itakamilika kama ilivoelekezwa na serikali.