Mkurugenzi wa Sheria na haki za binadamu wakili Anna Henga amesema kwamba
Sheria ya vyombo vya habari ilitakiwa kumalizika siku nyingi sana kwani tushawahi kufungua mpaka shauri katika mahakama ya Afrika Mashariki uamuzi wa mahakama hiyo ukaamua irekebishwe hivyo hivyo tuwaombe wabunge wetu kama Wadau muhuimu mwezi wa 11 mwaka huu watakapoijadili waipe kipau mbele.
Wakili Anna amewaomba wabunge kuangalia ibara ya kumi na nane katika katiba ambayo inatoa haki ya kutoa habari kupokea na kuchakata habari.
Wabunge kama Wadau muhimu wa habari wanao uwezo mkubwa wa kuangalia na kujadili sheria hii na kuona namna ambavyo inaweza kubadilishwa na kuboreshwa ili kuwawezesha waandishi wa habari kufanya kazi zao Kwa weledi
Aidha wakili Anna amesema kwamba mchakato huu ulitakiwa uwe umekamilika mapema kwani jitihada za kuomba kubadilishwa kwa sheria za habari zilianza kufanywa na wadau mbali mbali kwa muda mrefu sasa hivyo wabunge na serikali wanapaswa kuona hilo jambo na kulifanyia kazi ili kuweza kupata sheria nzuri katika tasnia ya Habari.
Baadhi ya sheria za habari zimekuwa kikwazo hapa na kusababisha wahariri na waandishi wa habari kushidwa kufanya kazi zao kwa weledi ambapo kwa sasa wahariri, waandishi na wadau mbali mbali wa habari wamekuwa wakiiomba Serikali ili kubadilishwa kwa Sheria hizo.