Waziri wa Habari na Technolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa.
……………………………….
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema Waziri wa Habari na Technolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari, wahariri pamoja na wadau mbali mbali wa habari ikiwa ni kujadili kwa pamoja sheria ya habari ya mwaka 2016.
Bw. Gerson msigwa amesema kwamba nia na madhumuni ya kikao hicho ni kupata msimamo wa pamoja kati ya Serikali na wadau wa habari kabla muswada huo haujapelekwa bungeni na waziri kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge na kupitishwa.
Aidha Msigwa Amesema kwamba Serikali ina dhamira ya dhati kuibadilisha sheria hiyo ili iweze kuwa bora zaidi ndiyo maana wameamua kushirikisha wadau wote ili waweze kutoa mapendekezo yao na kujadili vifungu ambavyo wanaona vina shida.
Ameongeza kuwa baada ya kikao hicho wadau hawatalalamika tena kwani watakuwa wameshirikishwa kikamilifu katika mabadiliko ya sheria hizo.
Kwa upande wake wa Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania ndugu Deodatus Balile amesema ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kupigania mabadiliko ya sheria za habari kwa kushirikisha wadau Wengine.