Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud akipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando kwa ajili ya ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko katika mipaka nchini katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika NIMR jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud akipongezwa na Dkt. George Mgomelle Mkurugenzi wa Mipango CDC mara baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka MDH.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud akizungumza katika hafla hiyo.
Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando akizungumza katika hafla hiyo na kutoa shukurani zake kwa wizara ya afya kwa kuonesha ushirikiano mkubwa.
Dkt. George Mgomelle Mkurugenzi wa Mipango CDC akizungumza katika hafla hiyo.
Picha za wadau mbalimbali wakiwa katika hafla ya makabidhiano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kuchangia jitihada za serikali katika kuimarisha huduma za afya mipakani, bandari na viwanja vya ndege ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko hasa yanayoambukizwa Katika hafla ya iliyofanyika NIMR jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo leo wakati alipomuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika makabidhiano ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 180 kwa ajili ya kuimarisha huduma za Afya katika mipaka, ili kujikinga na magonjwa ya milipuko na yanayoambukizwa.
“Vifaa hivi vina thamani kubwa na lengo ni Kuongeza mwitikio wa Taifa kwenye ufuatiliaji wa magonjwa ya kuambukiza katika mipaka ili kuhakikisha nchi imejiandaa vizuri dhidi ya magonjwa ya mlipuko na yanayoambukizwa” Amesema Prof. Said Aboud,
Prof. Said Aboud ameongeza kuwa Wizara ya Afya imepokea vifaa hivyo mbalimbali vya kielektroniki, vyumba vya uchunguzi (Booth), na Thamani (meza na viti) kutoka katika kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) kupitia shirika lisilo la kiserikali la MDH kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya katika mipaka na bandari na viwanja vya ndege nchini,
Naye Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando ameishukuru serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kutoa ushirikiano wa karibu na kufanikisha zoezi la utoaji wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kufuatilia tathmini na ukusanyaji wa takwimu kwa ili kuhakikisha nchi ina uwezo wa kuyakabili majanga hasa magonjwa ya mlipuko