Naibu Gavana wa Fedha na Uchumi wa Benki Kuu Tanzania Dk. Yamungu Kayandabila kulia na Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afrika (Frontclear) Bw. Philip Buyskes hati za makubaliano ya ushirikiano katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Fedha na Uchumi wa Benki Kuu Tanzania Dk. Yamungu Kayandabila kulia na Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afrika (Frontclear)Bw. Philip Buyskes wakibadilishana hati za makubaliano mara baada ya kusaini hati hizo za ushirikiano katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Fedha na Uchumi wa Benki Kuu Tanzania Dk. Yamungu Kayandabila akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini makubaliano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afrika (Frontclear) Bw. Philip Buyskes akizungumza katika hafla hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa benki za Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa City Benki, Geofrey Mchangila akifafanua baadhi ya mambo yanayohusu makubaliano hayo kwa upande wa mabenki.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Soko la fedha nchini Tanzania linatarajiwa kukua na kuwa na uhakika wa usalama wa kifedha hivyo kukuza mitaji kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine jambo ambalo litakuza ubora wa huduma za kifedha na kuchochea uchumi wa nchi kwa ujumla.
Hii inatokana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), kuingia makubaliano na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afrika (Frontclear) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kifedha ya nchini Uholanzi ambayo itatoa dhamana kwa taasisi za kifedha za ndani ili ziweze kukopesheka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa
Fedha na Uchumi wa Benki Kuu Tanzania Dk. Yamungu
Kayandabila, amesema BOT imeingia makubaliano hayo kwa niaba ya serikali ili kuzijengea uwezo taasisi za kifedha za ndani katika kumudu ushindani na kukuza uchumi.
“Nchi za SADC kama Uganda, Rwanda, Zambia, Ghana, Kenya ni wanufaika wa makubaliana hayo kwa mda mrefu ambayo ni fursa kwa kuwa taasisi zetu za fedha zitakuwa na dhamana ya uhakika na kujengewa uwezo wa kitaalamu wa kunufaika na masoko ya kifedha,”amesema,” Dkt. Kayandabila
Ameesema katika hatua hiyo kwa pamoja
watahakikisha benki zinamudu uwezo wa kukopa nje na
kujikopesha zenyewe huku taasisi hizo za kimataifa zikitoa
uhakika wa dhamana ili kuzifanya benki kuwa na usalama wa kifedha.
Amesema sekta kubwa ambazo ni benki zitanufaika zaidi kwakuwa kwa muda mrefu kulikuwa na matabaka baina ya benki kubwa na ndogo kushindwa kukopeshana au kuwekewa riba kubwa kutokana na dhamana hiyo sasa kila benki itanufaika sawa na nyingine.
Alisisitiza kuwa sekta za fedha nchini ikiwemo mifuko ya
hifadhi ya jamii na kampuni za bima pia zitahusishwa katika mpango huo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa benki za Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa City Benki,
Geofrey Mchangila, amesema makubaliano hayo yaliyosainiwa ni hatua kubwa ya kimapinduzi katika sekta ya fedha nchini.
Alisema soko la fedha kwa benki zaidi ya 45 nchini lilikuwa na changamoto ya kukosa dhamana hususani kwa benki za chini, kati na juu kukopeshana kwa muda mfupi.
Ameongeza kuwa katika mgawanyo huo wa benki tulikuwa hatuwezi kukopeshana sawa au kuwa na riba zinazofanana kutokana na kutoaminiana, lakini dhamana hii itasaidia kukua kimitaji kwakuwa benki ndogo inaweza kukopa sawa na benki kubwa kwa sasa kulingana na dhamana iliyopo,”alisema.
Mchangila, alisisitiza kuwa hali hiyo itakuwa chachu kwa benki hizo kuwa na uhakika wa usalama wa kifedha na kukuza mitaji