Ghala lililokuwa limehifadhia shehena za bidhaa za magendo ambazo zimeshindwa kulipiwa ushuru na wafanyabiashara limeteketea kwa moto katika Bandari ya Tanga huku chanzo hakijajulikana.
Ghala hilo linalomilikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tanga, lilikuwa na vitu mbalimbali yakiwemo mabalo ya vitenge 370, sukari, mchele, mafuta ya kupikia na pikipiki vilivyokamatwa vikiingizwa kwa njia magendo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba alisema alipata taarifa ya kuteketea kuwa ghala hilo linateketea kwa moto saa nane usiku na kufika eneo la tukio.
Alisema mkazo mkubwa ni kuhakikisha wanazima moto huo ndipo watafanya uchunguzi Ili kubaini chanzo kilichosababisha moto huo.
“Kwa Sasa jeshi la zimamoto na uokoaji wanaendelea na kuzima moto huo ndipo waendeleea kufanya uchunguzi Ili kubaini sababu za moto huo
“Kwa Sasa tunahakikisha usalama wa Mali zilizobaki Katika eneo hilo baada ya hapo tutaunda tume maalumu ya kufanya uchunguzi wa kina wa chanzo cha tukio hilo na sababu za kuzuka Kwa moto huo kabla ya kuchukuwa hatua zaidi,” alisema RC Mgumba.
Aidha alisema alitoa eneo hilo Octoba 17 mwaka huu ambapo ulikwenda alikagua shehena hiyo ya mabelo 370 na 170 zipo Mkinga alivikuta zipo sawa.
Naye Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Tanga, Fatma Ngenya alisema kuwa majira ya saa nane na nusu usiku walipokea taarifa za moto kutoka Mamlaka ya Bandari Tanga na walifanikiwa kufika eneo la tukio.
Ngenya alisema baada ya kufika eneo la tukio walifanikiwa kudhibiti moto huo huku akieleza kwamba kama wangechelewa kuzima athari zingekuwa kubwa sana
Naye kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema kwamba walipata taarifa saa name na nusu kupitia Afisa ulinzi Mwandamizi wa Bandari kwamba kuna tukio la moto alitoa kwake nyumbani na kukuta moto unaunguza katika ghala walilowapa watu wa TRA kwa ajili kuhifadhi mizigo walioshindwa kulipa wateja na iliyotaifishwa
Alisema kwamba baada ya hapo nao wakatoa taarifa kwa vyombo husika na juhudi ilifanyika huku akieleza suala hilo kwa sasa limeachiwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.