Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akikagua miundombinu ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya Isofu leo iliyopo Manispaa ya Sumbawanga ambapo ameagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa fedha. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akisalimiana na wananchi wa mtaa wa Mponda leo alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa zahanati yao iliyoanza kujengwa mwaka 2013 ambapo ameagiza ikamilike mwanzoni mwa mwaka 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na watalaam wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Matanga leo.
Sehemu ya majengo ya kituo cha Afya Mollo ambayo yamegahrimu shilingi Milioni 400 lakini mengine bado hayajakamilika hatua iliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)