Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Salim Said akizungumza wakati akifungua siku ya pili ya warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa marekebisho ya sheria za habari.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF wakifuatilia mjadala katika siku ya pili ya warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa marekebisho ya sheria za habari.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Salim Said amesema mwandishi wa habari akijua haki zake na sheria zinazoongoza tasnia ya habari ataweza kukutana na makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo wabunge na kuwashawishi juu ya sheria zinatatiza uhuru wa habari.
Ameutoa wito huo,Oktoba 21, 2022 wakati akifungua siku ya pili ya warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa marekebisho ya sheria za habari.
Ameongeza kuwa waandishi wa habari hapa nchini wanatakiwa kusoma sheria zinazohusu masuala ya habari na nyingine ili kujua namna ya kuzitekeleza na wajibu wao lakini pia wanapotaka zirekebishwe wawe na ushawishi mkubwa kwa watunga sheria na jamii.
“Bado waandishi hatujawa na uelewa mpana wa sheria zinazotuhusu, tufanye jitihada kuzijua. Tuwashawishi wenzetu juu ya sheria zinazokwaza ukuaji wa tasnia ya habari na maendeleo ya Taifa” amesema Said Salim
Naye Joyce Shebe Mhariri kutoka kituo cha luninga cha Clouds amesema anaamini wahariri wakijua namna ya kushawishi watunga sheria, sera na mipango ya Taifa watakuwa kwenye nafasi njema ya kuchochea maendeleo ya mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.