Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (aliyesimama), akihutubia katika hafla ya kupokea vitabu vya masomo ya sayansi nakala 786 kwa kidato cha tano na sita na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo. Mchango huo umetolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kama juhudi za kuiunga mkono Serikali katika kuhamasisha wanafunzi kusoma na kupenda masomo ya sayansi. Katika picha, wa pili kutoka kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Evaclotida Kapinga (kulia) na Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Arusha, Christopher Anyango (kushoto). Hafla hiyo imefanyika katika Shule ya Sekondari Mkata, Oktoba 18, 2022.
Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (GCLA), Evaclotida Kapinga (aliyesimama), akiwasisitizia jambo wanafunzi kuhusu umuhimu wa kusoma na kupenda masomo ya sayansi pamoja na kuwahimiza walimu kuendelea kutoa mchango wa elimu bora katika masomo ya sayansi.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika hafla ya kikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa vitendo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za wilaya ya Handeni. Vitabuna kemikali hizo zimekabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (katikati), Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa nne kutoka kulia) wakiwa pamoja na viongozi mbalimbali na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata (walioshika vitabu) mara baada ya kukamilisha hafla ya kukabidhi vitabu na kemikali kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Oktoba 18, 2022.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (aliyevaa koti la bluu bahari)), akikata utepe wakati akipokea vitabu vya masomo ya sayansi na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa Kaunda suti) Katika picha kushoto na kulia ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata.