Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza wakati wa kufungua Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya Ushirika wa akiba na mikopo Duniani.
Mwenyekiti wa Bodi ya SCCULT Dkt.Cuthbert Msuya akisoma risala kwenye Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya Ushirika wa akiba na mikopo Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mwanza.
Washiriki kutoka vyama mbalimbali vya ushirika wakiwa kwenye Maadhimisho
………………………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wakulima nchini wametakiwa kujisajali ili waweze kupata namba ya siri itakayowasaidia kununua mbolea kwa bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.
Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, wakati akifungua Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mwanza.
Alisema anafahumu kunachangamoto ya mawakala wa kuuza mbolea katika baadhi ya maeneo na Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kuongeza idadi ya mawakala kwenye maeneo ambayo yanaupungufu ili wakulima waweze kupata huduma ya kununua mbolea kwa ukaribu.
“Namba ya siri ndio silaha yako ukiitoa kwa mtu mwingine anaweza kununua mbolea kupitia namba yako hiyo nawewe ukapoteza fursa ya kuinunua mbolea ya ruzuku”, amesema Bashe
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya Ushirika vya akiba na Mikopo (SCCULT) Dkt.Cuthbert Msuya, amesema malengo ya Maadhimisho hayo ni kuwakumbuka na kuwaenzi waasisi wa ushirika wa akiba na mikopo kwa mchango wao mkubwa wa kueneza dhana ya ushirika pamoja na kuithamini mchango mkubwa wa vyama vya Ushirika wa akiba na mikopo katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Nchi mbalimbali Duniani.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Imarisha uwezo wako wa kifedha wa siku zijazo kupitia ushirika wa akiba na mikopo”
Msuya alieleza kuwa katika uendeshaji wa SACCOS nchini mafanikio mbalimbali yamepatikana ambayo ni kutengeneza fursa za uwekaji akiba kwa wanachama,ukopaji kwa Mashariti nafuu,ufikishaji wa huduma za kifedha katika maeneo ambayo taasisi nyingi za kifedha hazifiki na fursa za uwekezaji pamoja na maendeleo ya masuala mbalimbali ya kijamii.