NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAJUMBE
wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wameridhishwa na
uwekezaji uliofanywa katika kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Wilayani Lushoto
Mkoa wa Tanga.
wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wameridhishwa na
uwekezaji uliofanywa katika kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Wilayani Lushoto
Mkoa wa Tanga.
Wameyasema
hayo baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichoko Kata ya Mponde, jimbo la
Bumbuli Oktoba 15, 2022 ili kuona uwekezaji huo uliofanywa na Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

“Kwa niaba ya Kamati nichukue fursa hii kuwapongeza sana, nadhani nyuso zetu mmeziona
tumeridhika na kile tulichoona, naomba spirit hii mliyoanza nayo msiipunguze
muendelee nayo.”Alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Malima
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mpwapwa.
tumeridhika na kile tulichoona, naomba spirit hii mliyoanza nayo msiipunguze
muendelee nayo.”Alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Malima
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mpwapwa.
Alisema
kazi ya Kamati yake ni kuangalia pale ambako serikali imeweka mitaji.
kazi ya Kamati yake ni kuangalia pale ambako serikali imeweka mitaji.
“Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameruhusu fedha
nyingi kuja kwenye kiwanda hiki ili muweze kuwekeza na hivyo kutoa ajira za
kutosha na kuinua maisha ya Watanzania, hiyo ndiyo hasa nia ya Mheshimiwa
Rais.” Alibainisha.

Naye
Dkt. Julius Chaya ambaye ni Mbunge wa Manyoni na Mjumbe wa Kamati hiyo ya PIC
alisema wakati wawekezaji hao walipokutana na Kamati hiyo jijini Dodoma,
waliona wazo hilo la uwekezaji ni zuri sana kwani uwekezaji ndio umeweza kukuza
ajira kwenye maeneo mbalimbali duniani.

“Tunawapongeza
mnapofufua hivi viwanda, wananchi wanapata ajira, wakulima nao wanapata mahala
pa kuuza mazao yao kwakweli tunaishukuru serikali lakini pia tunaishukuru
Mifuko yote kwa kazi nzuri.” Alisisitiza Mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar
na Mjumbe wa Kamati, Mhe. Mariam Mwinyi.

Hata
hivyo baadhi ya wajumbe wametoa ushauri kuwa ni lazima uongozi wa kiwanda
uhakikishe wamejipanga vizuri katika eneo la masoko hususan yale ya nje, kwani
wanunuzi wakubwa wa bidhaa za kilimo licha ya kusisitiza ubora lakini pia
hupenda hakikisho la kupata bidhaa kwa mwaka mzima bila kusitisha.

Akiwakaribisha
kiwandani hapo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) Bw. Emmanuel Humba alisema wamefarijika sana na ujio wa Kamati kwani ni
ishara ya kutambua juhudi zilizofanywa na wawekezaji hao watatu.
“Kiwanda
hiki kama mlivyoona kinawahusu wananchi, wawekezaji tunaongeza nguvu tu, lakini
watakaofanya kiwanda hiki kifanye kazi ipasavyo ni wananchi wenyewe.” Alisema.
Alitoa
mfano kuwa wakati akiwa pale kiwandani alikutana na mkulima mmoja aliyeleta
majani yake ya Chai kilo 15 na alionyesha furaha sana kwani alisema baada ya
kuuza anauhakika wa kupata mahitaji mbalimbali ya nyumbani.
Aidha
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma alisema, kusudio kubwa la kukifufua kiwanda ni kuwawezesha
wananchi wa Lushoto, Bumbuli Korogwe na maeneo jirani kupata kipato na hivyo kuwainua
kiuchumi kwani wengi wanategemea zao hilo.
“Tunategemea
kwamba kiwanda kitanufaisha takriban asilimia 70 ya wakulima wa chai kutoka
Lushoto, Bumbuli Korogwe na maeneo jirani,” alifafanua Dkt. Mduma.
Akizungumzia hatua za utekelezaji wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda hicho, Bw. Anselim
Peter alisema awamu ya kwanza ya kufufua kiwanda hicho ilikuwa ni kukarabati
majengo na mitambo ambayo ilikufa kabisa, wakati awamu ya pili ilikuwa ni
kuboresha kiwanda kwa ujumla wake na kutengeneza menejimenti.
“ Karibu asilimia 100 kiwanda kimekamilika, tumeshaanza mchakato wa kuajiri wafanyakazi ili kusudi tunapoanza uzalishaji
kamili tuweze kutekeleza majukumu ya kiwanda ipasavyo.” Alisema.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Mitaji ya Umma, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe. George Malima (mwenye shati jekundu) wakiangalia hatua
mbalimbali za uchakataji chai kwenye kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Wilaya
ya Lushoto Mkoani Tanga Oktoba 15, 2022
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Mitaji ya Umma, wakipewa maelezo na Mwenyekiti w aBodi ya
Kiwanda cha Chai Mponde, Bw. Anselim Peter kuhusu hatua mbalimbali za
uchakataji chai kwenye kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Wilaya ya Lushoto
Mkoani Tanga Oktoba 15, 2022
Mwenyekiti
wa Bodi ya Kiwanda cha Chai Mponde, Bw. Anselim Peter (kushoto) akitoa
ufafanuzi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mitaji ya Umma na Menejimenti
za Mifuko ya WCF, PSSSF na Ofisi ya Msajili wa hazina kuhusu namna Boiler
linavyofanya kazi wakati wa ziara ya Kamati kutembelea kiwanda cha Chai Mponde
Oktoba 15, 2022