Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Benson Ndiege akizunguma katika kongamano la wanawake lililofanyika Malaika Beach Resort jijini Mwanza
Katikati Mheshimiwa Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula kiwaaga washiriki wa Kongamano la wanawake lililofanyika Jiji Mwanza,(kushoto Kaimu Naibu Mrajis Uhamasisha Bi Consolata Kiluma. Na kulia ni Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wanawake Monika Komba
Niabu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Mheshimiwa Antony Mavunde kitoka ukumbini kwa kuambatana na Waziri wa Aridhi Mheshimiwa Angelina Mabula
Mgeni Rasmi Mheshimiwa Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula akiongea na washiriki wa Kongamano la wanawake lililofanyika Jiji Mwanza leo tarehe 16/10/2022
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wanawake Monika Komba akielezea kwa Mgeni Rasmi Mheshimiwa Angelina Mabula kuhusu Kongamano la Wanawake. Na kulia ni Mwenyekiti wa Scullt Dkt Eng Cathbet Msuya akitetea jambo na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt Benson Ndiege
Washiriki wa Kongamano la Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waliohudhulia Kongamano hilo lililofanya Malaika Beach Resort.
Niabu Waziri wa wa Wizara ya Kilimo Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza katika kongamano la wanawake lililofanyika Jijini Mwanza leo tarehe 16/10/2022.
……………………………………..
Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Dkt. Angelina Mabula, amewataka wanawake walio katika Ushirika wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kuacha kuwa wanyonge badala yake wajikite kuwania nafasi za uongozi katika Vyama vya Ushirika.
Amesema idadi ya Wanaushirika Wanawake kwenye Sekta ya Ushirika ni kubwa lakini viongozi Wanawake kwenye Sekta hii ni ndogo sana.
Waziri Dkt. Mabula ametoa wito huo leo tarehe 16/10/2022 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake lililofanyika Malaika Beach Resort Jijini Mwanza litakaloambatana na Maadhimisho ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani yatakayofanyika mkoani Mwanza kuanzia tarehe 16 hadi 20/10/2022.
Mheshimiwa Dkt. Mabula amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika inatimiza majukumu yake ya Kisheria ya kuhakikisha wanaushirika Wanawake wanapatiwa elimu na mafunzo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Vyama vya Ushirika na umuhimu wa wanaushirika kuchukua nafasi za uongozi kwenye Vyama vyao.
Aidha, Mhe. Dkt. Mabula amewasisitiza Wanawake kupitia Ushirika kuwa waadilifu katika uchukuaji na urejeshaji Mikopo kwenye Vyama vyao kwani kutokufanya marejesho kwa wakati utadhoofisha uwezo wa kiuchumi wa Vyama vyao.
Aliendelea kuwasisitiza Wanawake kujitambua juu ya fursa zinazowazunguka, kujifunza namna ya kuzitumia vizuri katika wakati muafaka kwa Maendeleo yao kiuchumi na uimara wa Vyama vyao vya Ushirika wa Akiba na Mikopo pamoja na kuhakikisha wanaacha alama katika uongozi wao ndani ya Vyama vyao.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde, amewataka wanawake kujikita katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kupitia Ushirika. Pia amesisitiza uanzishaji wa SACCOS kwenye AMCOS uendelee kuhamasishwa na kuhimizwa kwani utasaidia kuimarisha uwezo wa Vyama hivyo kiuchumi na kuongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Naye Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika imejipanga kuwafanya wanawake kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia Vyama vyote vya Ushirika wa Kifedha na usio wa Kifedha.
“Hii itasaidia Wanaushirika wakinamama kujikwamua kiuchumi na kuwa na mitaji ya kutosha ambayo itawafanya waweze kutengeneza bidhaa zilizo bora ambazo zitaingia katika masoko makubwa,” amesema Dkt. Ndiege.