Mkurugenzi wa Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo kuhusu Tamasha Hilo litakalofanyika mkoani Mwanza Novemba 6, 2022.
Mkurugenzi wa Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo kuhusu Tamasha Hilo litakalofanyika mkoani Mwanza Novemba 6, 2022.
Tamasha la kuliombea Taifa la Tanzania linatarajiwa kufanyika Novemba 6, 2022 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi na muandaaji wa tamasha hilo ndugu Alex msama wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akiwaasa watu mbali mbali kutoka mwanza na mikoa ya jirani kufika kushiriki katika siku hiyo ya baraka ya kuliombea Taifa la Tanzania ili Mungu aweze kulilinda na majanga mbalimbali lakini pia kumuombea Rais wetu *Samia Suluhu Hassan* ili Mungu aweze kumlinda na kumuongoza katika kulisimamia Taifa la Tanzania.
Ameongeza kwamba katika tamasha hilo watakuwepo waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania, huku akiwataja baadhi yao kwa majina Rose Mhando, Christiana Shusho, Boniface Mwaiteje, Eveliny Wanjiru Kutoka Kenya naJoshua Ngoma Kutoka Rwanda
Aidha ndugu Msama amewaomba Watanzania wote kuungana pamoja katika siku hiyo kuliombea Taifa letu huku akiwasihi wakazi wa mwanza na mikoa ya jirani kufika mapema tarehe 6 kushiriki na kushuhudia Burundani kutoka wa waambaji mashuhuri watakaokuwepo siku hiyo.