Mratibu wa Mpango wa Miaka Kumi wa kumuenzi na kutangaza urithi wa Mwalimu Nyerere Adelaide Salema wakati akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere
Mkurugenzi na Muasisi wa magari ya kizamani Old Skuli Rider Tanzania George Joseph Msambure akizungumzia dhamira ya kuadhimisha Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kupitia msafara wa magari ya zamani
Wadau wa magari ya zamani (Oldschool ride Tanzania) wakipewa maelezo katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam wakati waliposhirikiana na Makumbusho ya Taifa kwa wamemuenzi Mwl. J.K. Nyerere kupitia msafara wa magari ya zamani yaliyozunguka katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya watalii ambao wametembelea katika Kijiji cha Makumbusho ikiwa ni katika kumuenzi Mwl. J.K. Nyerere leo Octoba 14,2022.
Aina mbalimbali za magari ya zamani ambayo yametumiwa na Wadau hao katika kumuenzi Mwl. J.K. Nyerere kupitia msafara wa magari ya hayo yaliyozunguka katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
……………………….
NA MUSSA KHALID
Watanzania wametakiwa kuendelea kumuenzi na kutangaza urithi wa Utamaduni wa Makumbusho ya Taifa ikiwa ni pamoja na mazingira,wanyamapori,madini na mali mbalimbali ambazo ni rasilimali za nchi yakiwemo magari yalitotumiwa katika harataki za uhuru.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Mpango wa Miaka Kumi wa kumuenzi na kutangaza urithi wa Mwalimu Nyerere Adelaide Salema wakati akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere ambapo wadau wa magari ya zamani Old Skuli Riders Tanzania wametumia siku hiyo kumuenzi Mwl. J.K. Nyerere kupitia msafara wa magari ya zamani yaliyozunguka katika mitaa ya hilo.
Adelaide amesema mwaka huu kutokana na mchango Mwalimu Nyerere kitaifa na kimataifa Wizara ya Maliasili iliandaa mpango wa miaka 10 wa kuenzi na kutangaza urithi ambapo wamefanya adhimisho la miaka 100 lakini pia wamefanya Mwalimu Nyerere Marathon.
Aidha Mratibu wa Mpango wa Miaka Kumi wa Kuenzi na Kutangaza Urithi wa Mwl Nyerere amewapongeza wadau wa magari ya zamani kwa kuamua kujitoa kumuenzi mwl. Nyerere kwa njia ya magari hayo.
Akizungumza Mkurugenzi na Muasisi wa magari ya kizamani Old Skuli Rider Tanzania George Joseph Msambure amesema magari hayo ya kizamani yanamchango mkubwa katika kuijenga nchini.
‘Tumeamua kuunga na na Makumbusho ya Taifa kumuenzi Mwl. Nyerere kwa njia ya msafara wa magari ya zamani kwani Uhifadhi wa magari haya ni njia mojawapo ya kumuenzi Mwl. Nyerere muasisi wa Taifa hili, yanatoa elimu na ajira kwa vijana, amesema Bw. Msambule
Wadau hao wa magari ya Kizamani awali wametembelea Kijiji cha Makumbusho,ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji hicho Agnes Robert amesema katika kijiji hicho pia kuna nyumba za Wazanaki jamii ambayo baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ametoka katika jamii hiyo.
Hafla ya Maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere imefanyika katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan amekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.