…………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameupongeza uongozi wa Wonderland Afrika na View Point Adventures Safaris LTD kwa ushirikiano waliouonesha wa kubuni Tamasha la Kiutamaduni la Kimasai linaloitwa Masai Festival kama zao jipya la Utalii wa Kiutamaduni.
Waziri Balozi Dkt. Chana ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Tamasha hilo Jijini Arusha alipo pewa nafasi ya kutoa Salamu za Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa takribani miradi ya Utalii wa Kiutamduni ipatayo 76 imeanzishwa katika maeneo mbalimbali hususan mikoa ya Kanda za Kaskazini, Pwani, Nyanda za Juu Kusini, pamoja na Kanda ya Ziwa ambapo jamii zinazoishi maeneo hayo zinajishughulisha na utalii wa utamdani
“Kufuatia mafanikio yaliyotokana na uandaaji na utangazaji wa filamu ya Tanzania – The Royal Tour chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, nchi yetu imeanza kupata ongezeko la wageni wanaotembelea nchini kwa utalii”. Aliongeza Mhe. Balozi Dkt. Chana
Mhe. Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa nchi inatarajia ongezeko zaidi la wageni wataofika nchini kwa miezi ijayo na kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo vya kiutamaduni.
“Natoa rai kwa Wadau na Mawakala wa utalii nchini kuongeza ubunifu hususan katika uandaaji wa vifurushi vya watalii ikiwemo maeneo yenye urithi wa utalii wa kitamaduni “ Amesisitiza Mhe. Balozi Dkt. Chana.