![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2022/10/IMG_20221008_093934_126-scaled.jpg)
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani –WHO Dr Zabulon Yoti wakati Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam baada ya kufanya mazoezi ya kutembea na kuongea ambayo wameyapa jina la Walk the Talk
Msimamizi wa Masuala ya magonjwa yasiyoambukiza WHO Dkt Alphonsina Nanai akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam baada ya kufanya mazoezi ya kutembea na kuongea ambayo wameyapa jina la Walk the Talk.
Baadhi ya wadau ambao wameshiriki katika mazoezi ya kutembea na kuongea ambayo wameyapa jina la Walk the Talk ambayo yamendaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO Nchini Tanzania.
……,……………….
NA MUSSA KHALID
Shirika la Afya Duniani WHO limewasisitiza watanzania kupenda kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na maradhi yasioyakuambukiza ikiwa ni pamoja na kuepukana na matatizo ya afya ya Akili.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani –WHO Dr Zabulon Yoti wakati akizungumza baada ya kufanya mazoezi ya kutembea na kuongea ambayo wameyapa jina la Walk the Talk ambapo amesema ufanyaji wa mazoezi unasaidia kuimarisha Afya.
Dkt Yoti amesema kuwa lengo lao ni kuonyesha umuhimu wa mazoezi jambo ambalo litawasaidia katika kukabiliana na maradhi mbalimbali.
Kwa Upande wake Msimamizi wa Masuala ya magonjwa yasiyoambukiza WHO Dkt Alphonsina Nanai amesema kuwa wamefanya mazoezi Ili kuonyesha kuwa ni muhimu lakini pia yanasaidia matatizo ya Afya ya Akili.
Dkt Nanai amesema magonjwa ya Akili yameongezeka Dunia nzima na yamesababishwa kutokana na hali ya maisha kuongezeka kwani gharama zimekuwa kubwa lakini pia na magonjwa yameongezeka.
“Mpaka sasa katika kila watu watano Mmoja alidhurika na hata kufikiri kujiua Kwa sababu ya matatizo ya Afya ya Akili kwa mfano ukiangalia COVID-19 matatizo ya Sonoma yaani Mtu anayesononeka yalikuwa yameongezeka kwa sababu katika kila watu 100 watu 26 walipata matatizo haya na mengine ya akili hii ni kwa mujibu wa takwimu za kimataifa”amesema Dkt Nanai
Aidha amesema kuelekea siku ya Matatizo ya Afya ya Akili Dunia Jumatatu OCT 10 Mwaka huu WHO inaendelea kuihamasisha Jamii kufanya mazoezi lakini pia kuangalia Afya zao mara kwa mara ili kujihadhari na maradhi.
Kwa Upande wao baadhi ya washiriki wa mazoezi hayo ya Walk the Talk wameipongeza WHO kuandaa mazoezi hayo kwani yanajenga kuimarisha Afya za watu jambo litakalosaidia kuweza kukabiliana na maradhi.