Mkurugenzi wa huduma za Biashara wa Wakala wa vipimo Deogratius Maneno akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani. Kwenye maonyesho ya tano ya kitaifa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.
Picha ya pamoja wakiwa katika banda la Wakala wa Vipimo WMA.
……………………………………….
Serikali kupitia Wakala wa Vipimo WMA imeendelea kusimamia jukumu lake Katika kuhakikisha mizani zinazotumika kwenye masoko maalumu ya kununulia madini katika maeneo mbalimbali hapa nchini zinakidhi viwango na watumiaji kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ili kumpa mlaji kilicho Bora.
Akizungumza kwenye maonyesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita Mkurugenzi wa huduma za biashara Wakala wa Vipimo WMA Ndugu Deogratias Maneno amesema kuwa lengo la Serikali kuanzisha utaratibu huo wa ukaguzi wa mizani ni kusaidia kuhakiki vipimo sahihi Katika maeneo mbalimbali nchini yenye masoko ya Madini.
Amesema mpaka hivi sasa kwa mkoa wa Geita kuna vituo vya mizani takribani vinane ambapo kuna mizani zinazotumika kununulia madini
Ameongeza kuwa wao kama WMA zoezi kubwa wanalofanya Kwa Sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wadogo ili kutambua faida na namna ya kutumia mizani walizonazo huku wachimbaji hao wakihimizwa kuwa waaminifu.
Pia amesema wana maeneo mapya ambayo wanayafanyia kazi kwa sasa ambayo ni ukaguzi wa mita za Majumbani zilizofungwa zamani na mita mpya ambapo amesema baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro wanashirikiana na Mamlaka ya maji na Wakala wa vipimo katika ukaguzi wa mita hizo za majumbani huku akiongeza kuwa katika mita za umeme pia wameanza kufanya ukaguzi hasa katika viwanda.