Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akiuliza jambo kwa msisitizo kwa Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita kwa ajili ya kujionea mkaa mbadala unaotengenezwa kwa kutumia makaa ya mawe hivyo kusaidia kuzuia ukataji wa miti kiholela na kutunza mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimsikiliza kwa makini Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Baadhi ya maofisa wa STAMICO wakiwa kwenye banda hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akipita maeneo mbalimbali katika banda hilo la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani.
Mabalozi wa Mkaa Mbadala wakiwa katika banda hilo kwa ajili ya kuhudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akiuliza jambo kuhusu utunzaji wa mazingira hasa kwa wachimbaji wadogo wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimsikiliza Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimnawisha maji Meneja Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena mara baada ya kupanda mti katika eneo la EPZA Bombambili mahali ambapo maonesho hayo ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akishuhudia wakati Meneja Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena alipokuwa akipanda mti katika viwanja vya EPZA Bombambili ambapo pia alitembelea banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani.
……………………………………..
Waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Suleman Dkt. Suleiman Jafo amelitaka Shirika la Madini la Taifa STAMICO kuongeza uzalishaji wa Mkaa Mbadala ili Mkaa huo uweze kupatikana kwa urahisi zaidi kwa wananchi nchi nzima ili kupunguza kwa kiasi kikubwa ukataji holela wa miti.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea kwenye banda la STAMICO katika maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita
“Ikiwezekana mviwezesha vikundi mbalimbali nchini kwa kuwapa mashine za kuzalisha Mkaa mbadala ili uweze kupatikana kwa urahisi kwa Watanzania wote na kwa haraka zaidi,”. Amesema Dkt. Suleiman Jafo
Ameitaka STAMICO Kuanza kutafuta Mawakala nchi nzima ili waweze kuanza kuuza Mkaa huo Mbadala mara utakapoanza kuzalishwa kwa wingi.
Dkt. Jafo amesema STAMICO inaweza kuwa mkombozi wa kuokoa rasilimali ya miti katika nchi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ili kwa pamoja waweze kuja na Kampeni ya pamoja ya kuzuia ukataji miti hovyo ambayo inaharibiwa kwa kasi kubwa na kusababisha uharibifu wa mazingira katika maoneo mbalimbali nchini.
Amehimiza vyombo vya ulinzi na usalama, Mashule, Vyuo na mashirika kuanza kutumia Mkaa Mbadala kama suluhisho la kupikia ili kuondokana na utumiaji wa kuni ambapo pia ameshauri TFS na STAMICO waanze kukutana ili kuweka mkakati na kujua, kuelewa na kufahamu namna Mkaa Mbadala unavyofanya kazi na unavyoweza kutumiwa.
Jafo ndiye alikuwa mgeni rasmi wa siku ya leo kwenye maonesho hayo ya madini yanayojumuisha zaidi ya makampuni 400 kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi ambapo moja ya mabanda aliyovutiwa nayo ni Banda la STAMICO.