Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe akizungumza na wafanyabiashara katika Soko la Magomeni alipofanya ziara kwenye soko hilo siku ya leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe akimsikiliza Mfanyabiashara wa mboga katika soko la Magomeni baada ya kufanya ziara kwenye soko hilo Leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe alitembelea na kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara wa soko la Magomeni.
………………………….
NA MUSSA KHALID
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe ametoa siku saba kwa Mkandarasi wa Manispaa ya Kinondoni kufanya kazi ya kuboresha miundombinu katika Soko la Kisasa la Magomeni ili kuwaondolea wafanyabiashara changamoto zinazowakabili.
Hayo yamejiri leo katika ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo aliyoifanya katika soko hilo kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali kwa wafanyabiashara hao ambapo wengi wamelalamika soko hilo kutokuwa na baadhi ya huduma muhimu ikiwemo ya maji.
Akizungumza na wafanyabiashara hao DC Gondwe amesema licha ya malalamiko ya wafanyabiashara hao pia walishatekeleza na kufanyika utatuzi wa wa baadhi ya Maeneo Katika Soko Hilo ikiwemo kutengeneza sehemu parking za magari,kujenga vibanda vya Wauzaji wa kuku lakini pia kuboresha Eneo wanalotumia mama lishe kufanyika shughuli zao.
“Serikali yenu ni sikivu kwani inalenga kuwasaidia wanachi wote kuna watu ambao Hapa wanadaiwa mpaka miezi saba lakini situmewavumilia hivyo muwe wavilivu kwani changamoto zote tunakwenda kuzitatua”amesema DC Gondwe
Aidha DC Gondwe ametumia fursa pia hiyo kutangaza kuuvunja uongozi wa soko la Magomeni baada ya uongozi kubainika kushindwa kutatua changamoto za wafanyabiashara sokoni hapo.
Katika Hatua nyingine Gondwe ameiagiza uongozi wa manispaa ya kinondoni kupitia kitqqqqqengo cha TEHAMA kulitangaza soko ilo ili lijulikane na kusaidia kuongeza wateja katika soko hilo.
Kwa Upande wa Wafanyabiashara hao kwa nyakati tofauti wamelalamikia kuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa wateja,ukosefu wa maji sokoni hapo, ikiwa ni pamoja na kukosa manunuzi ya jumla katika soko hilo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Hanifa Hamza,amesema ofisi yake itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyasha Ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Hata hivyo Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameambatana na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Kinondoni,wakuu wa Idara,Pamoja na Meneja wa Dawasa.