Na Mwandishi wetu – Geita
Wakati Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini kwa mwaka 2022 yakiendelea katika viwanja wa uwekezaji (EPZA) Mkoani Geita ambayo yanashirikisha Kampuni, Wajasiriamali ,Mashirika na Taasisi mbalimbali za binafsi na Serikali ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)na wananchi kwa ujumla ambapo wanachama wa NSSF wameonekana kufurahia elimu na huduma kutoka NSSF.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao waliotembelea banda la NSSF wamesema wamefurahishwa na huduma walizopata katika banda hilo ikiwemo elimu jinsi ya kutumia mifumo mbalimbali ya kidigitali kama vile programu (Applications) za _’Employer Portal na Member Portal, NSSF Taarifa, NSSF Whatsapp chat bot’_ zinazomuwezesha mwanachama na mwajiri kupata huduma popote pale alipo jambo ambalo litawapunguzia gharama na usumbufu wa kwenda katika Ofisi za NSSF.
“Nimefurahia Maonesho na pia nimejifunza mambo mengi katika banda la NSSF,nilikuwa sielewi namna ya kuangalia taarifa zangu kwenye simu lakini leo nimepata elimu hiyo na kwamba itapunnguza gharama na usumbufu wa kwenda kwenye ofisini kwao, kwakweli NSSF imejipanga huduma zao ni nzuri hivyo nitoe wito kwa wananchi wanakuja kutembelea maonesho hayo wasisite kuja katika banda la NSSF” alisema Henry Mwinuka, mwanachama wa NSSF.
Naye Mpuzi Msumbuko,Mwanachama wa NSSF alisema kuwa alifika katika banda la NSSF kuangalia taarifa za michango yake hivyo amefurahi kuzipata.
“Nimekuja hapa kuangalia taarifa zangu za michango kama mwajiri wangu ananiwekea katika Mfuko,sasa nimekuja hapa katika Maonesho nikadhani ni bora nije kuangalia taarifa za michango yangu nimekuta ziko vizuri mwajiri wangu anaweka michango yangu kwakweli nimefurahi na nimeridhika na huduma nilizopata hapa“ Alisema Mpuzi Masumbuko.
Licha ya Mfuko kutoa huduma mbalimbali za Hifadhi ya Jamii, Mfuko una sajili wanachama wapya baada ya kuwapatia elimu kupitia mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa sekta isiyo rasmi ambapo wananchi waliojiari wenyewe wakiwemo wachimbaji wadogo wadogo wa madini kupata fursa ya kujiwekea akiba ya baadaye.
“Nimekuwa na shauku ya kujiunga na NSSF kwa kipindi kirefu sana ila nilikuwa sijapata nafasi ya kutembelea katika Ofisi zao lakini kwa sababu ya Maonesho haya ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini hapa Mkoani Geita nimeona ni fursa kwangu kuja katika banda la NSSF kuja kujiunga na hivyo nashukuru nimefanikisha adhma yangu ya kuwa mwanachama wa NSSF kwahiyo kuanzia sasa nitaanza kujichangia kwa hiari ili nijiwekee akiba hii ni kama kibubu cha kisasa sio kama kile kilichokuwa nyumbani mwisho wa siku kinabomolewa” alisema Festus Mluli ambaye ni mwanachama mpya wa NSSF
Maonesho hayo yenye kauli mbiu ‘Madini na fursa za kiuchumi: Ajira kwa Maendeleo Endelevu’, yalianza tarehe 27 Septemba 2022 na yanatarajiwa kuisha ifikapo tarehe 8 Oktoba 2022 hapa mkoani Geita.