Mhifadhi daraja la kwanza anayesimamia idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo Bw.Semistockles Bita akizungumzia safari ya kwenda katika kisiwa cha Rubondo katika banda la Maliasili kwenye maonesho ya madini mkoani Geita leo Jumanne Oktoba 6,2022.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Pellagy Richard Marando Afisa Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Gombe mara baada ya kutembelea katika banda la Maliasili kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita leo Oktoba 4,2022.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akimshukuru Bw.Pellagy Richard Marando Afisa Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Gombe mara baada ya kupokea zawadi alipotembelea katika banda la Maliasili.
…………………………….
KATIKA Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Hifadhi ya taifa ya Kisiwa cha Rubondo imeandaa safari ya kutoka kwenye Maonesho hayo kuelekea kwenye Hifadhi hiyo kwaajili ya kufanya Utalii kuona mambo mengi yanayopatikana kwenye hifadhi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye Maonesho hayo leo Oktoba 4,2022 Mhifadhi daraja la kwanza anayesimamia idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo Bw.Semistockles Bita amesema safari hiyo imetengeneza package ambapo mtu mzima atalipa elfu 30 na watoto watalipa elfu 15 na malipo hayo yanajumuisha usafiri wa kwenda na kurudi, kufanya utalii lubondo na kupata chakula cha mchana.
“Tunachukua nafasi hiii kuwahamasisha watu wote ambao wapo hapa Geita na waliopo jirani ili waungane pamoja nasi kutembelea hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo tarehe 6,2022 na safari itaanzia kwenye viwanja vya maonesho vya Bombambili”. Amesema
Aidha amesema wameweka bei ambazo ni nafuu ambazo watu wengi wanaweza kuzimudu ili mwisho wa siku kila mtanzania aweze kupata nafasi ya kutembelea hifadhi hiyo ambayo imekuwa na vivutio vingi.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akipata maelezo kutoka kwa Bw.Pellagy Richard Marando Afisa Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Gombe mara baada ya kutembelea katika banda la Maliasili kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita leo Oktoba 4,2022.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akimuuliza swali Bw.Pellagy Richard Marando Afisa Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea katika banda la Maliasili kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita leo Oktoba 4,2022.
Muonekano wa Banda la Maliasili katika picha.