Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO Meja Jenerali Michael Isamuhyo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya tano ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita.
Mtambo wa Kisasa wa Kuchoronga na kutoa sampuli kwa ajili ya tafiti mbalimbali za madini katika maeneo ya migodi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Meja Jenerali Michael Isamuhyo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Lucas Selelii wakijadiliana jambo na Simon Shayo Makamu wa Rais wa Kampuni ya GGM wakati alipotembelea katika banda la kampuni hyo kwenye maonesho ya madini mkoani Geita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Meja Jenerali Michael Isamuhyo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Lucas Selelii wakiangalia machapisho walipotembelea banda la TEITI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Meja Jenerali Michael Isamuhyo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Lucas Selelii wkatika banda la Tume ya Madini.
……………………………………
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewataka wananchi pamoja na makampuni makubwa yanayohusika na masuala ya madini kuutumia mtambo wa kisasa wa uchorongaji wa RC utakaowapatia taarifa sahihi na kurahisisha huduma kwa urahisi.
Akizungumza wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho ya madini Mkoani Geita Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi STAMICO Meja Jenerali Michael Isamuhyo amesema mtambo huo ni wa kwanza Tanzania kwani unafanya kazi kwa kutumia rimoti.
Meja Jenerali Michael amesema mtambo huo wa kisasa wa uchorongaji na utafiti wa madini aina Reverse Circulation ( RC) ni bora kwani hata waendeshaji wake ni tofauti na mitambo mingine ambayo imekuwa ikitumia nguvu za binadamu.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Bodi SATMICO amesema uchorongaji ndio njia pekee inayosaidia kupata taarifa na data sahihi za kiwango cha madini kilichopo katika maeneo mbalimbali hasa madini aina ya dhahabu.
Amesema kupitia Maonyesho hayo wameweza kuonyesha vifaa ambavyo STAMICO wanavyo lakini pia wamewaelimisha wananchi juu ya masuala madini kwa ujumla na teknolojia.
‘STAMICO kwa sasa inakwenda kuzuri zaidi kwani tunatumia teknolojia ya kisasa katika mitambo mbalimbali tuliyonayo ambayo watu wengi hasa wachimbaji wadogo wanashughulika nayo’amesema Meja Jenerali Michael
Hat ahivyo amepongeza uwepo wa maonyesho hayo na kushauri kuwa ni vyema yakaendelea kufanyika kila mwaka na hata katika mikoa ambayo haina madini kwani yatasaidia wananchi kufika na kujifunza kuhusu shughuli za madini zinazofanywa.