Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe (kushoto),Mtoto Alberto Revocatus , Mwandishi wa Vitabu vya Watoto Bi. Anitha Martine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakizindua kitabu cha mimi ni nani? (Who Am I?) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Mwandishi wa Kitabu Cha Auntie Anitha’s Charms Bi. Anitha Martine akitoa ufafanuzi kuhusu maudhui ya kitabu chake kipya cha mimi ni nani? (Who Am I?) katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliyofanyika jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe (wa pili kutoka kushoto), Mtoto Alberto Revocatus, Mwandishi wa Kitabu Cha Auntie Anitha’s Charms Bi. Anitha Martine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mimi ni nani? (Who Am I?).
Jaji Dkt. Modesta Opiyo (kutoka kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe, Mshauri wa Masuala ya Jinsia, Afya ya uzazi na ulinzi wa watoto Dkt. Katanta Simwanza wakifatilia matukio ya uzinduzi wa kitabu cha mimi ni nani? (Who Am I?) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
……………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali imesema itaendelea kutoa ushirikiano kwa waandishi wa vitabu wanaoandika maudhui yenye lengo la kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo malezi ya watoto katika kuhakikisha wanajengewa uwezo wa kujiamini na kufikia malengo tarajiwa katika maisha yao.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mimi ni nani? (Who Am I?) kilichoandika na mwandishi Anitha Martine, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe, amesema kuwa vitabu venye maudhui mazuri ya kuisaidia jamii ni rafiki kwa Taifa katika kuleta maendeleo
Mhe. Gondwe amempongeza mwandishi wa kitabu cha mimi ni nani? (Who Am I?) Anitha Martine kwa kuandika kitabu ambacho kinakwenda kuwa msaada kwa wazazi, walimu pamoja na watoto katika kufikia ndoto zao za kimaisha.
“Jukumu letu ni kuhakikisha kitabu cha Who Am I? kinawekwa katika mfumo wa audio na vitual na maudhui yake yanapaswa kuwekwa katika mitandao ili tuweza kuwafikia makundi mengi katika jamii” amesema Mhe. Gondwe.
Amesema kuwa usomaji wa vitabu kuna msaidia mtu kuweza kujiamini na kupata elimu ambayo itamsaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
“Nilisoma kitabu kimoja kilinisaidia kuweza kujiamini na niligundua hakuna mtoto mjinga duniani, hivyo tuna kazi ya kubadilisha kizazi hiki kama alivyofanya Auntie Anitha’s” amesema Mhe. Gondwe.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu vya aina mbalimbali kwa ajili ya kupata maarifa ambayo itawasaidia katika kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Mshauri wa Masuala ya Jinsia, Afya ya uzazi na ulinzi wa watoto Dkt. Katanta Simwanza, amesema kuwa wakati umefika wa kuanza kuwekeza kwa watoto ili kupiga hatua katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Amesema kuwa kitabu mimi ni nani? (Who Am I?) ni rafiki kwa ajili ya makunzi ya watoto, hivyo kila mazazi anapaswa kuwanacho kwa ajili ya kumsaidia mtoto wake.
Mwandishi wa Vitabu vya Watoto Bi. Anitha Martine, amesema kuwa Kitabu Cha Auntie Anitha’s Charms kinalenga kumsaidia mtoto katika kujiamini, kujitambua pamoja na kuelewa mazingira ambayo yanamzunguka.
Bi. Martine amesema kuwa mtililiko wa kitabu cha Auntie Anitha’s Charms kinakuja na vitabu vingi, lakini kitabu cha kwanza ambacho kipo sokoni kinaitwa mimi ni nani ? (Who Am I?).
Amesema kuwa kitabu cha ‘Who Am I?’ kinamuangalia mtoto mdogo ambaye anakwenda kujitafuta yeye ni nani, ambapo anaaza kujiuliza yeye mwenyewe na kuwauliza wazazi wake.
“Swali hili mmi ni nani ? ni swali fikilisha sana hata kwa watu wakubwa, lakini lengo ni kumpa mtoto changamoto katika kujitambua yeye ni nani” amesema Bi. Martine.
Amefafanua kuwa walengwa wa kitabu cha Who Am I ?’ ni wazazi, watoto, walimu na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha wanaweza kuwasaidia watoto wao katika kufikia ndoto zao za kimaisha.
Amesema kuwa kitabu ‘Who Am I ?’ kinamsaidia mtoto kuweza kuwasiliana vizuri na mzazi wake na mazazi kuweza kumuelewa vizuri mtoto wake.
“Kitabu kitamsaidia sana mzazi katika kumjua zaidi mtoto wake na mtoto kujitambua na kuweza kujiamini, kitabu kinapatikana katika maduka yote ya vitabu pamoja na mitandao wa Amazon pamoja na maduka yote ya vitabu hapa nchini” ”amesema Bi. Martine.