Mkuu wa kitengo Cha sheria katika Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la LST mara baada ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali unaofanyika jijini Dodoma.
…………………………….
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAHITIMU wa shahada ya sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili binafsi nchini, wamehimizwa kufanya mafunzo kwa vitendo kupitia Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) ndani ya mwaka mmoja.
Hayo yamesemwa leo Septemba 29,2022 na Mkuu wa kitengo Cha sheria katika Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la LST mara baada ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali unaofanyika jijini Dodoma.
Bi.Mollel amesema lengo la taasisi hiyo ni kutoa mafunzo Bora na stahili ya uanasheria kwa Vitendo,utafiti na ushauri elekezi katika masuala ya sheria kwa watu stahiki.
“Dhamira kuu ya taasisi hii ni kutoa ushauri wa kisheria kwa watoto,kutoa ushauri wa kisheria kwa wanawake,kuandaa nyaraka za mahakamani, kufuatilia mwenendo wa kesi mahakama kutoa mwongozo wa taratibu za kufuatilia kesi, kutoa msaada wa kisheria katika makundi mengine sambamba na usuluhishi wa migogoro”amesema Mollel
Amesema kuwa toka kuanzishwa kwa taasisi hiyo imeweza kupata mafanikio kama wahitimu wa taasisi wamekuwa wakiorodheshwa/kusajiliwa kama mawakili wa kujitegemea na wengine wakiajiriwa katika utumishi wa umma kama mawakili wa Serikali au mahakimu wakazi.
Aidha wahitimu wengine wanaendelea kukamilisha taratibu za kuwa mawakili wa kujitegemea ili waanze kufanya kazi kwa weledi.
“Kuna watu wanatoka vyuoni moja kwa moja wanakuwa hawafahamu namna ya kufanya kazi hizi kwahiyo Taaisi yetu sisi inawapa mafunzo lengo ni kuwajengea uwezo mawakili hawa ili waliendelee kutekeleza majukumu yao.”amesema Mollel.