Na Alumanus Mwasenga
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewataka wasimamizi wa majengo ya Utumishi kuboresha miradi ya nyumba ambayo imewekwa kwa aajili ya kuendelea kuwlinda na kuwathamini wastaafu wa serikali.
Ameyasema hayo wakati akitembelea jengo la Shirika la Watumishi Housing Company TD lililopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam lenye (Apartment 88) Huku likiwa na vyumba ya biashara na nyumba za kupangisha kwa ajili ya makazi lengo likiwa kuwasaidia wastaafu kuhusu changamoto za makazi zinazowakabili.
“Maeneo ambayo ningependa Kuona yanafanyiwa kazi vizuri ni yale yanayotoa motisha kwa umma,lakini pia yale yanayotatua changamoto zinzowakabili wastaafu Wlwetu wanapomaliza kulitumikia taifa” Amesema Mh. Jenista Mhagama
Aidha Mh. Jenista amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na shirika hilo katika uuzaji wa nyumba zake baada ba kukuta (Apartment) zote za jengo Hlhilo zimenunuliwa na watumishi wa umma hasa wakati alipokagua baadhi ya maeneo ili kujihakikishia na kujua hatua iliyofikiwa.
“Nimefurahi sana leo nimekuja kutembelea mradi huu wa magomeni,Apartment 88 zote zimenunuliwa na watumishi wa umma nimekagua mpaka huko ndani,nyumba nzuri bora na kwakweli zinawafaa watumishi wa umma”
Hata Hlhivyo Mhagama ametoa wito kwa Mlmaafisa utumishi wanaoshughulika na utumishi wa umma kuwaunganisha watumishi wao kwa Shirika la Watuishi Housing Ili nawao waweze kupata fursa zinazopatiakana katika taasisi hiyo.
Pascal Masawe ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Watumishi Housing amesema kuwa watajitahidi kuhakikisha watumishi ambao wapo katika utumishi wa umma waweze Klkunufaika na mradi huo kutoka Watumishi Housing.
“Lengo letu hasa ni kuhakikisha watumishi walioko katika halmashauri mpya wanapata nyumba za gharama nafuu”