Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Chukuzi, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Usafiri majini wametoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo usafiri kwa njia ya maji katika viunga mbalimbali vya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Wadau hao walitembelea na kutoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la TASAC, usalama wa abiria katika vyombo vya usafiri kwa njia ya maji, fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji ikiwemo ufadhili wa masomo yanayohusu kesta hiyo ikiwa ni moja ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Bahari Duniani.
Wadau walitembelea Shule ya Sekondari Kilwa, Kivinje, Ilulu, Kikanda, mialo ya Kilwa Kivinje, Somanga pamoja na Kisiwa cha Songosongo na Nyuni.