Mkurugenzi wa shirika linalojishughulisha na sanaa za maonyesho nchini Tanzania -ASEDEVA kizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la Kimataifa la Muziki wa Asili la Marafiki Music Festival 2022 linalotarajiwa kufanyika kuanzia tar 6 – 8 Oktoba mwaka huu.Meneja wa Tamasha la Marafiki Music Festival 2022 Upendo Manase akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu shughuli zitakazofanyika Tamasha la Kimataifa la Muziki wa Asili la Marafiki Music Festival 2022 linalotarajiwa kufanyika kuanzia tar 6 – 8 Oktoba mwaka huu.Muandaaji wa Singeli Festival Masoud Kandoro ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Kimataifa la Muziki wa Asili la Marafiki Music Festival 2022 linalotarajiwa kufanyika kuanzia tar 6 – 8 Oktoba mwaka huu.
……………………..
NA MUSSA KHALID
Takriban wasanii 200 wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha la Kimataifa la Muziki wa Asili la Marafiki Music Festival 2022 linalotarajiwa kufanyika kuanzia tar 6 – 8 Oktoba mwaka huu.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa shirika linalojishughulisha na sanaa za maonyesho nchini Tanzania -ASEDEVA Isack Abeneko amesema kuwa lengo la Tamasha hilo pia ni kuleta wadau na wataalam mbalimbali wa sanaa kubadilishana uzoefu na ujuzi wao na wasanii ili kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali za sanaa na ubunifu wao.
Amesema Tamasha hilo limekuwa likikua kwa kasi kwani limeweza kutengeza ajira kwa vijana 125 kwa kipindi cha miaka mitatu jambo ambalo limewezesha vijana pia kujipatia ujuzi wa elimu pamoja na kufahamu biashara ya Muziki.
Abeneko amesema Marafiki Music Festival wanajikita katika kuwekeza mafunzo ya muziki biashara na masoko ili kuboresha thamani na mwanga katika sanaa ya muziki kuweza kujhipatia uzoefu mkubwa.
‘Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 – 8 Oktoba 2022 katika viwanja vya Makumbusho/ Village Museum Kijitonyama jijini Dar es salaam kuanzia saa Na tarehe 9 Oktoba 2022 litahamia Firefly Bagamoyo huko Bagamoyo dhamira yetu pia ni kuleta wadau na wataalam mbalimbali wa sanaa kubadilishana uzoefu na ujuzi wao na wasanii ili kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali za sanaa na ubunifu wao’amesema Abeneko
Aidha amesema kabla ya Tamasha kutafanyika shughuli mbalimbali ikiwemo Marafiki Extra,kufanya usafi Hospitali ya Mwananyama,kufanya matembezi kutoka ASEDEVA mpaka Kijiji cha Makumbusho.
Naye Meneja wa Tamasha la Marafiki Music Festival 2022 Upendo Manase amezitaja shughuli nyingine zitakazofanyika kuwa tar 7 Oktoba kutakuwa na warsha ya Mbinu ya Kuunganisha muziki wa Jadi na wa Kisasa,tar 8 kutakuwa na suala la Uchapishaji na Hati miliki itakayoongwa na mzee Kitime na pia kutakuwa na majadiliano kati ya wasanii na wadau wa muziki.
Kwa upande wake Muandaaji wa Singeli Festival Masoud Kandoro amewahamasisha wananchi kuendelea kuupenda utamaduni wao hivyo amewtaka kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Tamasha la Marafiki Music Festival limeandaliwa na ASEDEVA na kufadhiliwa na Firefly Bagamoyo kwa kushirikiana na Nafasi Art Space, Alliance Française – Dar es salaam, Ubalozi wa Ufaransa – Tanzania, Singeli festival, Acto Lights, MuDa Africa, We present label, Hip Hop Asili Festival, Sauti za Busara, Ongala Music Festival, Ajabu Ajabu, DCMA Zanzibar, BASATA na Wizara ya Utamaduni.
Ikumbukwe kuwa ASEDEVA imeweza kuanzisha matamasha/events za kila mwaka likiwemo Tamasha la Kimataifa la Ngoma la Haba na Haba (Haba na Haba International Dance Festival) na Tamasha la Muziki la Marafiki (Marafiki Music Festival).