Nahodha wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Gadafi Chambo akitoa maelezo kwa Mhe. Atupele Mwakibete (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi alopotembelea banda la TASAC wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, Leo tarehe 26 Septemba, 2022, Wilayani Kilwa.
Mhe. Atupele Mwakibete (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi akijadili jambo na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Bi.Stella Katondo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, Leo tarehe 26 Septemba, 2022, Wilayani Kilwa.
Mhe. Atupele Mwakibete (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi akihutubia wananchi waliofika katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani.
Mhe. Atupele Mwakibete (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali
……………………………….
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete ametoa wito kwa wadau wa shughuli za usafirishaji kwa njia ya maji kuzingatia utunzaji wa mazingira ya bahari, maziwa na mito.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani wilayani kilwa amesema jambo hilo linawezekana kufanikiwa kwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa inayosimamia usafiri salama na endelevu duniani kote.
Aidha aliongeza kuwa Tanzania ina eneo kubwa la maji ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika. Eneo la bahari pekee kutoka kwenye ufukwe hadi kufika katika eneo la bahari kuu ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 223,000. Ukiacha eneo la ukanda wa Bahari ya Hindi, pia yapo Maziwa Makuu ambapo Kaskazini kuna Ziwa Victoria, Magharibi Ziwa Tanganyika na Kusini magharibi kuna Ziwa Nyasa.
Maziwa hayo kwa pamoja yana jumla ya eneo la kilomita za mraba 64,500. Kuna maziwa mengine mengine madogo madogo, mito na mabwawa ambayo shughuli mbalimbali za kiuchumi zinaendesha kwa ajili kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha, Tanzania ina eneo refu la ufukwe wa bahari la Km. 1424.
Maeneo haya ya maji ni muhimu kwa uchumi wetu na kama yatatumiwa kwa kuzingatia viwango vya usafiri salama vinavyostahili na kuzingatia utunzaji wa mazingira na rasilimali zilizopo, yatakuwa na faida kubwa sana kwa jamii zetu kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.
Mhe. Mwakibete alieleza kuwa takribani asilimia 80 ya biashara za kimataifa kwa ukubwa na takribani asilimia 70 ya biashara ya kimataifa kwa thamani husafirishwa kupitia kwa meli kupitia bahari.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya bahari duniani Wilayani Kilwa Naibu Waziri Atupele Mwakibete amesema kwa kutambua umuhimu huo Serikali inatekeleza mradi wa Ujenzi wa meli nane zikiwemo nne kwa Tanzania Bara na Nne Visiwani Zanzibar.
“Napenda kuwahakikishia Viongozi wetu wa kitaifa wanatambua umuhimu mkubwa wa Usafiri huu na uwekezaji huo ukikamilika utakuwa na manufaa kwa kuongeza pato lakini pia kupuunguza gharama za bidhaa zinazosafirishwa’ Amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu Waziri Mwakibete amesema pamoja na ujenzi wa meli Serikali kwa Tanzania Bara inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali wa miundombinu ya bandari za Habari ya Hindi na Kwenye maziwa lengo likiwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria.Mwakibete ameongeza kuwa Serikali Kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendelea kukagua vyombo vya usafiri majini ili kuhakikisha usaalama wa abiria na mizigo unazingatiwa wakati wote.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bi Zawadi Kawawa ameipongeza Serikali kwa kuendeleza miundombinu yna kusema kukamilika kwake kutarahisisha usafirishaji wa bidhaa zinazozaliwa mkoani humo na itakuza utalii.Mkuu wa Wilaya Kawawa maeishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendeleza bandari ya uvuvi ya Kilwa ambayo kukumilika kwa mradi huo kutasafirisha tani elfu 60 kwa mwaka
Naye Muwakilishi wa Katibu Mkuu wa Uchukuzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Stella Katondo amemuhakikisha Naibu Waziri Mwakibete kuwa Wizara itaendelea kufatilia kwa karibu shughuli za usafiri wa majini kwa kuzingatia miongozo ya Kimataifa.
Maadhimisho ya siku ya bahari yanafanyika kwa siku nne Mkoani Lindi ambapo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya “Teknolojia mpya kwa uchukuzi baharini wa kulinda mazingira’