Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Muliro Muliro
………………..
NA MUSSA KHALID
Jeshi la Polisi kanda Maamlum ya Dar es salaam limemkamata Tazarn Alfan Mwambengo (27), mkazi wa Ukonga, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu kifo cha Dkt. HARRISON MWAKYEMBE kupitia chaneli ya televisheni ya mtandaoni jambo ambalo si la kweli.
Akitoa taarifa kwa wanahabari Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Muliro Muliro amesema kuwa mtuhumiwa huyo Katika chanel hiyo ya aliandika “BREAKING NEWS HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKYEMBE”.
Aidha Kamanda Muliro amesema baada ya Mtuhumiwa huyo kusambaza taarifa hizo ziliibua taharuki kubwa kwa wananchi hasa kwa Dkt Mwakyembe mwenyewe na familia yake.
Katika Tukio jingine Kamanda Muliro amesema Jeshi hilo limemkamata Innocent Adam Chengula, Mhehe, 23, mkazi wa Kigogo Luanga,kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Dkt. HASSAN ABBAS Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao na kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.
‘Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, vifaa hivyo ni kama ifuatavyo: 1. Kompyuta mpakato (laptop)1 2. Simu 3, 3. Mike ya kutangazia, 4. Modem 1, 5. Kadi za simu za mitandao mbalimbali 9 zenye usajili wa majina tofauti’amesema kamanda muliro
Jeshi la Polisi limetoa rai kwa Watanzania kuchukuwa tahadhari wakati wa kutuma pesa au kufanya miamala kwa njia ya simu ili kuepuka kutapeliwa, Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa watu wote watakao vunja sheria, kanuni na miongozo inayoelekeza matumizi sahihi ya mitandao