………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana, ameshiriki Ibada ya Maadhimisho ya Jubile ya Miaka 50 ya Utume wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Parokia ya Mlagali, Mkoani Njombe
Katika ibada hiyo iliyoambatana na Sherehe za maalum za Maadhimisho hayo, Waziri Balozi Dkt. Chana ameupongeza WAWATA kwa kazi nzuri wanayoifanya katika ulezi wa Kanisa na jamii kwa ujumla.
Aidha Waziri Balozi Dkt Chana ameongeza kuwa Serikali chini ya Kiongozi mwenye upendo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameoa mikopo kwa Wanawake isiyo na riba hivyo amewashauri WAWATA kuchangamkia fursa hiyo.
Awali katika Mahubiri yake Paroko wa Kanisa Ladislaus Mgaya ametoa wito kwa akina mama kuendelea kuwa walimu wa Imani, Matumaini, mapendo na Ukarimu kama sehemu ya Utume uliotukuka katika Kanisa na jamii kwa maana akina mama ni nguzo ya kanisa.