………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kwala
Sep 21
WIZARA ya Maji imebariki kibali cha matumizi ya sh.bilioni 20 zitazopeleka maji katika eneo la Kwala, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Ridhiki Shemdoe ambae ni Katibu Mkuu TAMISEMI, aliyasema katika ziara Maalumu ya kukagua kazi zinazoendelea za kukamilisha Mradi huo.
“Wizara ya Maji tayari imeshatoa kibari cha matumizi ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 20, zitazopeleka maji kwenye Jiji la Kibiashara la Kwala, lengo kuhakikisha Mradi huo unakuwa na miundombinu yote,” alieleza Shemdoe.
Kwa upande Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi John Kijazi alipongeza kuhudi za ujenzi wa Jiji hilo, huku akiwataka wataalamu kutoka Wizara hizo kujiongeza katika kubiresha Jiji badala ya kufungwa na yaliyokuwa kwenye makabradha.
Gabriel Joseph Katibu Mkuu Uchukuzi aliuhakikishia msafara huo kwamba Mradi, utakamilika kama ilivyopangwa.
“Magari yote yatayoleta makontena hapa nchini yataishia hapa Kwala, yanayokwenda nchi za nje pia yatachukuliwa hapa, yakitokea Dar es Salaam yakiletwa kwa Treni,” alisema Gabriel.
Ally Gugu Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara alipongeza Serikali kwa Uwekezaji huo, unaolenga kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.
Mhandisi Telchemis Mramba aliwapongeza wataalamu kutoka Wizara hizo, ambao wamepiga kambi Kwala kufanikisha kukamilika kwa Mradi huo.
“Niwapongeze Wataalamu wetu kwa kazi mnayoendelea kuitekeleza hapa Kwala, tunataraji zoezi ili litakamilika kama ilivyopangwa na Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu,” alisema Mramba.
Awali mmoja wa Wataalamu kutoka TAMISEMI Miringay Joseph, aliwaelezea makatibu hao namna kazi zinavyokwenda, huku wakieleza kwamba itakamilika kama ilivyopangwa.
MWISHO.