Mlemavu wa uziwi kutoona Mwanaasha Abdalah akizungumza na waandishi wa habari Katika ofisi za Shirika la Vijana wenye ulemavu –YoWDO jijini Dar es salaam.Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa la Sense International Frank Jakson akieleza namna wanavyowasaidia watu wenye ulemavu wa uziwi kutoona.
…………………….
NA MUSSA KHALID
Serikali imeombwa kutekeleza mwongozo iliyotoa ya kuwapatia watu wenye ulemavu mikopo wakiwa katika kikundi cha watu wawili au mmoja badala ya watano ili waweze kunufaika na mikopo hiyo.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na vijana wenye ulemavu wa uziwi kutoona wakati wakizungumzia changamoto wanazokumbana kuwa ni pamoja na mwongozo huo mpya wa kupatia mkopo kutotekelezwa.
Akizungumza Mlemavu wa uziwi kutoona Mwanaasha Abdalah akifasiriwa na Mtaalamu wa Lugha ya alama Protus Mwalongo amesema kutokana na kundi hilo kusahaulika kwenye jamii imesababishwa kutoshirikishwa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
‘Mikopo ya Halmashauri ya 2% imekuwa ikiwanufaisha watu wenye ulemavu lakini viziwi wasioona bado hawajapata manufaa yake kwa sababu kuna masharti ambayo ni vigumu kutekeleza kwa upande wetu viziwiwaioona’amesema Mwanaasha
Aidha Mwanaasha amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kwa jamii kutoamini kuwa viziwi wasiona wanaweza kujitegemea na kujihusisha katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa la Sense International Frank Jakson amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika kuwasaidia watu wenye ulemavu wa uziwi kutoona ili waweze kupata mahitaji yao muhimu ikiwemo kuwapatia elimu.
Jakson amesema kupitia mradi wao wa Wezesha vijana umeweza kuwapatia mafunzo na mitaji vijana 33 wenye ulemavu wa uziwi na kutoona ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujipatia kipato.
Aidha Serikali imeendelea kutoa fursa ya mikopo ya asilimia 2 ili wenye ulemavu na wao waweze kupata fursa ya kufanya shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha na wao kuchangia katika pato la taifa.
Hata hivyo Taasisi ya Sense Internationa Tanzania kupitia mradi wa WEZESHA VIJANA kwa kushirikiana na Shirika la Vijana wenye ulemavu –YoWDO imewapatia mafunzo ya ujasiriamali na mtaji vijana wenye uziwi kutoona.