………….
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesaini mkataba wa miaka mitatu (3) wenye thamani ya Dolla laki tano (5) za Kimarekani na shirika la Ford Foundation.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa Leo na THRDC imeelezwa kuwa Mkataba huo wa miaka mitatu (2022-2024) umelenga kusaidia Utekelezaji wa Mpango mkakati mpya wa Mtandao (2023- 2027) hususani katika utekelezaji wa dhima na maono ya mtandao yanayolenga kuhakikisha kunakuwa na mazingira huru, salama na rafiki kwa shughuli za utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.
Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi leo Septemba 20, 2022 na utekelezaji wake utaanza mapema mwezi huu na kumalizika mwaka 2024.