Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akisikiliza kero zinazowakabili wazee wa Wilaya ya Mbinga kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Makita mjini Mbinga.RC Thomas yupo katika ziara ya kusikiliza kero zinazowakabili wazee katika wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma
baadhi ya wazee katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Kigonsera wilayani Mbinga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas baada ya kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee.
……………….
adiwani waagizwa kusimamia miradiMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali itaendelea kutafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wazee zikiwemo kutoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee.
Kanali Thomas ametoa ahadi hiyo wakati anazungumza na wazee Pamoja na madiwani wa Wilaya ya Mbinga kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa sekondari ya Kigonsera na sekondari ya Makita mjini Mbinga.
RC Thomas ametoa rai kwa wazee kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili wanazifikisha kwenye Baraza la Wazee la Mkoa wa Ruvuma ambalo limezinduliwa hivi karibuni ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.
“Serikali ya Awamu ya Sita ipo tayari kusikiliza na kushughulikia kero mbalimbali za wazee,pia nawaasa vijana hakikisheni mnawahudumia wazee wenu ili mpate baraka kwa sababu wazee ni kudni muhimu ambalo limesahaulika katika jamii ’’,alisisitiza Kanali Thomas.
Ameagiza huduma za afya kuboreshwa katika dirisha la kuhudumia wazee katika kila kituo cha kutolea huduma za afya ili wazee waweze kupata huduma za matibabu kwa haraka.
Mkuu wa Mkoa pia amewaasa wazee kutumika kutatua migogoro inayojitokeza katika jamii na kwamba wazee wanatakiwa kuwa washauri wakuu katika jamii hali ambayo italeta amani na utulivu na vijana kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa wazee.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza madiwani wa Halmashauri zote kuwa walinzi wa miradi inayotekelezwa katika Kata zao ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha zilizotumika kwenye miradi husika.
Ameagiza viporo vya miradi ambayo haijakamilika kwa muda mrefu kuhakikisha wanaisimamia na inakamilika ndani ya muda mfupi ili wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.