…………..
Adeladius Makwega-MAKOLE
Jumatano ya septemba 14, 2022 nilipokuwa katika shughuli zangu nilikutana na mama mmoja shabiki mkubwa wa Yanga akiwa amevalia kilemba chekundu, blauzi nyekundu suruali nyeusi na viatu vyekundu.
Kwa hakika bila ya kuingiza unazi wa Simba na Yanga, mama huyu alikuwa amependeza mno, kama unavyofahamu msomaji wangu rangi nyekundu inavutia sana na kuonekana hata ukiwa umbali gani, bahati hiyo siyo kwa rangi ya kijani au njano.
Kwa kumtazama bi mkubwa huyu alipendeza zaidi kwani alikuwa na mweusi wa asili unaong’ara huku rangi ya blauzi nyekundu ikiwakawaka katika sura yake iliyopambwa na mafuta yanayonukia vizuri sana mithili ya tausi aliyepo katika bustani ya mfalme.
Kwa ujuavyo msomaji wangu mwanakwetu si mwingi wa uchoyo, nimejaliwa ukarimu, nilimsogelea ndugu yangu huyu kwanza na kumpa mkono wa hongera uliojaa pongezi tele za kupendeza huko, nayeye alijibu kwa neno asante. Nikauliza mambo haya ya kupendeza ni ya lini au siku zote? Nilijibiwa kuwa hizo ni habari za siku zote.
Nilipomdodosa nilibaini kuwa kupendeza huko kote mama huyu alikuwa mzaliwa wa Mtaa wa Twiga wa Jangwani Dar es Salaam huku akishabikia timu ya mtaa huo ya Yanga African Sports Club ya.
Kwa kuwa mwanakwetu ni shabiki wa Simba niliomba ruhusa ya kupiga picha na mama huyu huku nikiwa na langu la moyoni, nilijibiwa sawa lakini unataka kupiga picha je mume wake akiuliza huyu uliyepiga naye picha ni nani je akatoe majibu gani? Niliulizwa
Nikamwambia hilo tu, kabla sijasema neno akaniambia unataka nipewe talaka? Nikamwambia unaogopa talaka, talaka ni karatasi tu, nikamjibu akitoa talaka ninakuhamishia Chamwino Ikulu, utakuja kupigwa na upepo wa Ikulu ya Chamwino ambao kwa sasa marashi ya Zanzibar yananukia. Akasema thubutu, nikamwambia ndiyo nakwambia.
Shabiki huyu wa Yanga akaniambia sawa lakini mtu mwenyewe wa kanisani kila jumapili mambo ya mitala utayaweza? Nikamjibu nitamshirikisha Padri wangu, akanijibu mpaka ukamshirikishe. Wewe nihakikishie hapa hapa mimi nikiachika nije Chamwino Ikulu, alisema.
Kumbe mama huyu kwa chonjo walikuwepo vijana wake kadhaa ambao pia ni mashabiki wa Yanga wakinitazama kwa jicho kali, mmoja wapo akauliza sasa mzee mama yetu unamuhamishia Chamwinbo Ikulu kwenye marashi ya Zanzibar, nikajibu naam, Je mustakabali wa sisi watoto wake utakuwaje?
Mama mtu alisema hapo wanangu umemuuliza swali sahihi kabis, huyo baba yenu mtarajiwa..
“Wewe tumekusikia ukipanga mikakati ya mama peke yake sisi wana je, tupe mustakabali wetu.” Niliulizwa. Niliwaamia hawa wtaoto wajitahidi kuwa na heshima na mie baba yao kwanza ili nimalizane na mama yeo.
Mama huyu akasema kuwa kama unataka picha basi kwanza tumalizane na mkataba wa wanangu , ili likitokea la kutokea na kama ulivyowasikia wanangu wameshasikia mimi na wanangu tutayafuata marashi ya Zanzibar yaliyopo Chamwino Ikulu pumzi unayo niliulizwa
Mwanakwetu sikupata bahati ya kupiga picha hiyo, Septemba 15, 2022 nimekutana na mama huyu kavaa nguo zake za rangi ya kijani na njano nilimtazama kwa jicho pembe lakini nilibaini hakupendeza kabisa, hata ile habrai ya kumuhamishia Chamwino Ikulu nimeighairi.
Yeye akininanga kuwa nitaendelea kula wa chuya kwani nimeshindwa masharti nanikipenda boga nipende na maua yake.
makwadeladius @gmail.com
0717649257