Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mh. Dk. Khalid Salum Mohamed akifunga Kongamano la Wataalamu wa Hali ya Hewa Barani Afrika na Ulaya lililokuwa likifanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 16,2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk. Agnes Kijazi akitoa hotuba yake ya shukurani mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo leo kwenye ukubi wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 16,2022.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Dk. Ally Possi akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Dk. Khalid Salum Mohamed ili kufunga kongamano hilo.
Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk.Mariane Diop Kane akizungumza katika kongamano hilo wakati alipokuwa akitoa salam zake kutoka (WMO).
Mwakilishi wa Shirika la EUMESAT kutoka Jumuiya ya Ulaya Vincent Gabaglio akitoa salam zake na shukurani kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha kongamano hilo ambali lilikuwa muhimu zaidi katika masuala mazima ya utabiri wa hali ya hewa na namna ya kutumia taarifa za hali ya hewa kwa bara la Afrika.
Mwakilishi wa Shirika la EUMESAT kutoka Jumuiya ya Ulaya Vincent Gabaglio kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Dk. Ally Possi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika ufungaji wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk. Agnes Kijazi kushoto na Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk. Mariane Diop Kane wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa kongamano hilo.
Matukio ya Picha mbalimbali zikionesha washiriki wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja