Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Health Promotion Tanzania -HDT Dr Peter Bujari wakati akizungumzia na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu uchangiaji wa mfuko wa Kimataifa wa UKIMWI,Kifua Kikuu pamoja na Malaria.
…………………….
NA MUSSA KHALID,
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Health Promotion Tanzania -HDT limeishauri serikali ya Tanzania kuchangia mfuko wa Global Fund kama Nchi Nyingine Ili kusaidia mapambano ya magonjwa ya Ukimwi,Kifua Kikuu Pamoja na Malaria.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dr Peter Bujari wakati akizungumzia uchangiaji wa mfuko wa Kimataifa wa UKIMWI,Kifua Kikuu pamoja na Malaria.
Amesema kuwa Global Fund imesaidia kupunguza maambukizi mapya,ikiwa ni pamoja na kuwapatia matibabu wagonjwa hivyo kupunguza vifo na kuwezesha wengi kushiriki shughuli za uzalishaji mali na maendelea ya nchi kwa ujumla.
Aidha Dr Bujari amesema kuwa ili kufikia malengo ya kutokomeza maradhi ya kifua Kikuu na Ukimwi kwa miaka mitatu ijayo,zinahitajika Dola za Kimarekani Billion 130.2 na Global Fund peke yake inahitaji Dola Bill 18.
‘Kwa nchi yetu ya Tanzania pekee,Global Fund imeweza kuachangia kiasi cha Dola za Kimarekani Bill 2.6 toka mwaka 2002 ambapo zimesaidia kupambana na magonjwa ya Kifua Kikuu,Ukimwi na Maleria na zaidi ya watu milioni 1.2 waliweza kupata huduma za dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi,Zaidi ya watu Mill 8.2 wamepata huduma na kupona Maleria’amesema Dr Bujari
Dr Bujari amesema kuwa baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikichanguia mfuko huo ni pamoja na Afrika ya Kusini,Kenya,Benin,Namibia,Senegal,Lesotho,Cote D’Ivoire,Togo na Zimbabwe na hivi karibuni Uganda imeonyesha nia ya kuchangi hivyo ni vyema na Tanzania ikashiriki katika kuchangia mfuko huo.
Amesema wakati umewadia sasa wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan kuchangia Mfuko wa GlobaL Fund kama nchi nyingine zinavyoweza kujitolea.
‘Kidunia Mkutano Mkuu wa uchangiaji wa Mfuko kwa Awamu ya 7 utafanyika nchini Marekani kuanzia tar 19 -21 septemba mwaka huu ambapo fedha hizo zinategemewa kuokoa Maisha ya wanadamu zaidi ya Million 20 duniani kote ifikipo mwaka 2026’ameendelea kusema Dr Bujari
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Health Promotion Tanzania –HDT ilianzishwa mwaka 2012 kwa malengo ya kusaidia kuboresha afya na maendeleo ya watu nchini Tanzania.